The House of Favourite Newspapers

Novatus Dismas: Nimetimiza Ndoto ya Kucheza na Samatta Ulaya

0

BAADA ya kufanikiwa kulamba dili la kusajiliwa na Klabu ya Macabi Tel Aviv inayoshiriki Ligi Kuu Israel kiungo kinda aliyekulia Azam FC, Novatus Dismas amesema ndoto yake ya kucheza Ulaya na straika wa Taifa Stars na Fernabache Mbwana Samatta sasa itatimia.

 

Novatus amesema kupata nafasi ya kusajiliwa na kwenda kucheza kwenye klabu ambayo huwa inapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kitu kikubwa kwake kwa sababu anakwenda kuongeza idadi ya wachezaji wanaocheza ligi kubwa wakitokea Tanzania, baada ya Samatta kuwakilisha kwa miaka mingi.

 

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Azam FC Thabit Zakaria alitoa taarifa juzi Alhamisi kuwa kiungo huyo aliyekulia kwenye akademi ya timu hiyo amepata nafasi ya kusajiliwa na Macabi Tel Aviv baada ya kufuzu majaribio ya muda mfupi akiwa na timu ya vijana na wakubwa na kisha makubaliano ya siri kufi kiwa baina ya pande zote mbili katika uhamisho wa kinda huyo aliyecheza Biashara United kwa mkopo msimu uliopita.

 

“Kupata nafasi ya kufuzu majaribio na kusajiliwa na Macabi Tel Aviv, kwangu nahesabu kama kutimiza ndoto ya kucheza na Samatta Ulaya kwa sababu Israel japo haipo Bara la Ulaya ila huwa inatoa timu moja kwenda kucheza UEFA na hii klabu ni moja ya timu ambazo ushiriki mara kwa mara mashindano hayo hivyo naamini msimu ujao naweza kuwepo kwenyen ligi hiyo.

 

“Kwahiyo sasa Tanzania huenda ikawa na wachezaji wawili watakaonekana katika ligi kubwa za Ulaya kama Mungu ataendelea kutubariki. Nawashukuru sana Azam FC, Biashara na timu zote ambazo zimenisaidia kufi ka hapa na Watanzania wote ambao wanatuombea dua ndugu zao ili tufanikiwe kupitia soka.”

Issa Liponda, Dar es Salaam

Leave A Reply