Nyoka wa Maonyesho Aua Mtu Katavi

JAMES PASCHAL, mkazi wa Mtaa wa Kilimani Kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, ambaye ni mtaalam wa sanaa ya kucheza na nyoka, amefariki dunia baada ya kung’atwa na nyoka, wakati akiwa porini akijaribu kuwakamata kwa ajili ya kazi yake.

 

Akizungumzia tukio hilo, mdogo wa marehemu, Jefta Paschal,  aliyeambatana naye porini kwa ajili ya mawindo, amesema  walifanikiwa kumkamata nyoka huyo na wakiwa katika harakati za kumweka kwenye mfuko wa sulphate, ndipo marehemu aling’atwa mkononi.

 

Baadhi ya majirani wa marehemu wamesema kuwa marehemu alifika nyumbani kwake akiwa katika hali mbaya na kuamuru kupelekwa hospitali, lakini ghafla hali ilibadilika na kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.

 

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilimani, Florence Mbabule, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuwaasa wananchi kuacha kuchezea wanyama wakali kama nyoka.

 


Loading...

Toa comment