The House of Favourite Newspapers

Obama Aomboleza Kifo cha Bibi Yake

0

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amesema yeye binafsi na familia yake wanaomboleza kifo cha bibi (nyanya) yao, Sarah Ogwel Onyango Obama, ambaye anafahamika na wengi kama “Mama Sarah” lakini anayefahamika katika familia kama “Dani” au Granny.

 

Katika ujumbe wake wa Twitter ulioambatana na picha yake akiwa na Mama Saraha Obama alipoitembelea Kenya kwa mara ya kwanza, Bw Obama amesema ‘’Tutamkosa sana, lakini tutasherehekea kwa shukran maisha yake marefu’’.

Bibi wa Kambo wa Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, Sarah Obama amefariki katika hospitali nchini Kenya akiwa na umri wa miaka 99, familia yake imenukuliwa na vyombo vya habari vya nchini humo. Mama Sarah amekuwa mgonjwa kwa muda na amefariki alipokuwa akipokea matibabu.

 

Leave A Reply