The House of Favourite Newspapers

Omotola Atamba kukutana na Jesse Jackson!

Omotola Jalade na Jesse Jackson.

Na ANDREW CARLOS| GAZETI LA IJUMAA| KUTOKA NAIJA

NAIJAMKONGWE wa filamu ambaye pia ni mhamasishaji wa amani Afrika, Omotola Jalade amejitamba kwa kuanika picha nyingi na ‘komenti’ za kutosha akiwa na mchungaji na mhamasishaji wa amani wa kimataifa, Jesse Jackson.

Omotola alikutana na Jesse katika mkutano mkuu wa kuhamasisha amani na haki za binadamu uliotayarishwa na Crans Montana, Dakhla nchini Morocco ambapo alialikwa kama mmoja wa wageni watakaozungumza.

Hata hivyo, baada ya kumalizika kwa mkutano huo, Omotola alipiga naye picha nyingi na kuziachia mtandaoni huku akitamba kukutana na mhamasishaji aliyekuwa akimuota na kwamba bahati imekuwa ya kwake pekee kama staa wa Nigeria. Omotola ambaye pia ni mama wa watoto wanne, alikuwa ameambatana na mumewe, Captain Ekeinde.

 

Comments are closed.