The House of Favourite Newspapers

Onyango alia na sanaa Bongo

0

Mzee Onyango (1)

Msanii mkongwe wa vichekesho nchini, Issa Joseph ‘Mzee Onyango’ akipozi ndani ya studio za Global TV Online leo.

Mzee Onyango (2)

Mzee Onyango akipozi na Mhariri Msaidizi wa Gzeti la Ijumaa Wikienda, Gabriel Ng’osha.

Mzee Onyango (3)

Mzee Onyango akiwa na Nyemo Chilongani wa GPL

Mzee Onyango (4)

Boniphace Ngumije wa Global akiwa katika pozi na Mzee Onyango kwenye studio za Global TV Online.

Mzee Onyango (5)

Mzee Onyango na Mtangazaji wa Global TV Online, Shorvieny Mohammed katika pozi.

MKONGWE wa filamu za vichekesho na tamthilia Bongo, Issa Joseph, Onyango amelilia sanaa ya Bongo kuwa na mfumo mmoja kitu kinachosababisha kushindwa kuendelea mbele.

Akizungumza na Global TV Online leo ndani ya Mjengo wa Global Publishers, Onyango alisema kuwa kitu kinachoididimiza sanaa ya filamu Bongo ni waandaaji kung’ang’angia kuwa na mfumo mmoja.

“Utakuta mwandishi wa filamu ni huyohuyo, leo anaandika filamu hii kesho anapewa tenda ya kuandika filamu nyingine kwa hiyo anaandika kama ile mwisho wa siku filamu zote zinafanana,” alisema Onyango.

Kujua zaidi juu ya mahojiano ya Global TV Online na Mzee Onyango, usikose kutembelea www.globaltvtz.com

Leave A Reply