The House of Favourite Newspapers

Penzi la Wolper na Rich Lipo Saiti

0

MWANAMAMA wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper au Mama P amefunguka mazito juu ya penzi lake na baba wa mtoto wake, Rich Mitindo.

Wolper amesema; “Penzi liko site (saiti), ogopa sana penzi likiwa katika hatua hiyo na nilitoa tahadhari kwa sababu kuna wadada wengine hawana heshima huyu mpenzi wangu Rich alikuwepo singo karibia mwaka mzima na miezi sita sikumkuta na mwanamke.

“Tulikutana China ndiyo tukaanzisha mahusiano mwaka 2016, tukaachana na baada ya kuachana hatukuwa maadui na nilijishangaa kuwa na rafiki ambaye ni ex wangu, lakini kumbe ni Mungu tu ni mtu ambaye amepangwa kuwa baba mtoto wangu.

“Tulirudiana mwaka jana ndiyo akapatikana mtoto wetu P. Kwa hiyo unapomwona mtu ana mtu wake, halafu unataka kumkomesha Jac ndiyo maana narudia ile sentensi kwamba sitodili na baba mtoto wangu.

 

“Nitadili na wewe ambaye unajua huyu ni mtu wangu namposti na yeye ananiposti, halafu unakuwa naye hata kama amekufuata kwani hujui kama ni mwanaume wa mtu? Kuwa na heshima..” anasema Wolper akionekana kupaniki ile mbaya.

Leave A Reply