The House of Favourite Newspapers

Polisi Ni Watu Na Jamii Ni Polisi Tushirikiane Kwa Pamoja Kutokomeza Ukatili Na Uhalifu

0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Agustino Senga.

Waamini wa Kanisa la Moraviani lililopo Majengo mjini Tunduma wilayani Momba kwa Mchungaji Japhet Nyangwa wametakiwa kuendelea kutoa huduma ya kiroho huku Jeshi la Polisi likiendelea kutoa huduma ya kimwili ya kulinda raia na mali zao kwa lengo la kutekeleza kazi ya Mungu kwa kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia na uhalifu katika jamii.

Rai hiyo ilitolewa April 07, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Agustino Senga wakati alipohudhuria katika ibada ya jumapili kanisani hapo na kutoa elimu kuhusu madhara ya ukatili na uhalifu yanayotokea katika jamii.

Kamanda Senga amesema “Jeshi la Polisi limeendelea na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia vinatokomezwa katika jamii hivyo wazazi/walezi mnatakiwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa ya vitendo hivyo pindi muonapo au mfanyiwapo ikiwa ni pamoja na kuendelea kufanya doria za kiroho ili jamii ibadilike na ichukie vitendo hivyo kwa lengo la mkoa wetu kuwa salama” alisema Kamanda Senga.

Aidha, Kamanda Senga aliongeza kuwa “Mnapaswa kuwasimamia watoto wadogo kwani kwa umri walionao hawawezi kujisimamia na kufanya maamuzi, wanahitaji njia na miongozo ili waweze kufikia malengo ya masomo yao sasa basi mzazi/mlezi ni jukumu lako na jamii kwa ujumla kuwaongoza watoto kwa yale yaliyo mema kama kumfundisha na kuja naye kanisani ili amjue Mungu mapema kwa kufanya hivyo tutatengeneza kizazi kilicho bora na kisicho na mmomonyoko wa maadili katika taifa letu”

Sambamba na hilo, Kamanda Senga amewataka waumini wa Kanisa hilo kutumia maneno kutoka kwenye Biblia Takatifu kuwakumbusha waumini hao kuacha kutoa rushwa kwa watumishi wa serikali kupitia Kutoka 23:8 “Nawe usipokee rushwa, kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki”.

KIJANA AKUTWA na SARATANI ya PUA INAKIMBILA KWENYE UBONGO – ANAPUMULIA MDOMO – ALIA AKISIMULIA…

Leave A Reply