The House of Favourite Newspapers

Polisi Yakamata Watuhumiwa 100 Madawa ya Kulevya Dar

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro akizungumza na wanahabari.

Akisikiliza kwa makini maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari.

Akionesha magari mawili yaliyokamatwa kwenye oparesheni hiyo.

Akionesha moja kati ya silaha zilizokamatwa kwenye oparesheni hiyo.

JESHI la Polisi jijini Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 100 wa madawa ya kulevya katika maeneo mbalimbali ya jiji kutokana na oparesheni inayoendelea hivi sasa.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa kuanzia Februari 25, mwaka huu mpaka Machi 1, mwaka huu kutokana na oparesheni kali inayoendelea ya kupiga vita na kupambana na wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya nchini.

“Aidha, katika oparesheni hii ambayo ni endelevu, jumla ya kete 413 za dawa za kulevya zimekamatwa, puli 50 na misokoto 86 ya bangi pamoja na pombe haramu ya gongo ipatayo lita 43,” alisema.

Pia ameeleza kuwa  jeshi hilo limefanikiwa kukamata majambazi 12 wa unyang’anyi wa kutumia silaha jijini hapa katika oparesheni iliyofanyika maeneo mbalimbali ya jiji, kuanzia Februari Mosi, 2017 ambapo majambazi hao wamekuwa wakitumia pikipiki (bodaboda) katika kutekeleza azma yao hiyo ya uhalifu.

Alieleza kuwa katika mahojiano ya awali, majambazi hao wamekiri kutumia silaha katika matukio ya ujambazi pamoja na kuua na kujeruhi na tayari upelelezi unaendelea, utakapokamilika wote watafikishwa mahakamani.

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.