Q Chief Aanika Waliombadili Kwenye Muziki

MSANII wa Bongo Fleva, Q Chief, ameeleza kuhusu safari ya maisha yake kwenye muziki wakati alipokutana na msanii Jose Chameleone nchini Uganda ambapo alimpokea na kumuonyesha baadhi ya vitu walivyokuwa pamoja.

 

Q Chief amesema: “Nilipokuwa nchini Uganda msanii Chameleone Jose alinikaribisha vizuri na kunizungusha kila kona, hii ilitokana na heshima na upendo tuliokuwa nao.

 

Aidha akizungumzia kuhusu maendeleo yake ya kimuziki tangu alipoanza hadi sasa amesema: “Ustahimilivu ndiyo unanijenga kuwa imara siku zote, nimekutana na watu sahihi kama Daxo Chali na Marco Chali ambao wamefanya mabadiliko kwenye muziki wangu.

 

“Nafanyia kazi Albamu yangu mpya na tour yangu ambayo itakuja, kwa hiyo watu wajiandae kunipokea, mimi ni msanii ambaye napenda kuingia kwenye damu ya mtu na hiyo ndiyo maana ya mwanamuziki na muziki mzuri,” amesema Chilla.

 

Q Chief ni mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao mpaka sasa wana heshima zao kwenye muziki na bado wanafanya muziki.

 

Toa comment