The House of Favourite Newspapers

Rais Kenyatta Atoa Wiki Mbili Tatizo la Mahindi Mpakani Litatuliwe – Video

0

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata ametoa wiki mbili kwa watendaji serikalini kuhakikisha sakata la mahindi ya Tanzania yaliyozuiwa kuingia Kenya linapatiwa ufumbuzi.

 

Kenyata ametoa agizo hilo leo Jumatano Mei 5, 2021 mjini Kenya katika kongamano la wafanyabiashara mbele ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

 

Hivi karibuni mahindi ya Tanzania yalizuiwa kuingia Kenya ikidaiwa kuwa na sumu kuvu jambo lililosababisha malori kukwama mpakani huku wafanyabiashara wakihaha kusaka maeneo mengine ya kuuza bidhaa hiyo.

 

Katika maelezo yake leo Kenyatta amesema Kenya na Tanzania ni nchi jirani na ndugu, hakuna sababu ya kuwekeana vikwazo vitakavyoumiza wananchi.

 

“Natoa maelekezo hapa, kwanza yale mahindi yaliyolala mpakani waziri nakupa wiki mbili hilo suala liwe limeisha, mahindi yote yawe yamefunguliwa na maneno yaishe kwa sababu hatutaki kuumiza watu wetu,”

 

“ Pili mawaziri wanaohusika nendeni kutatua foleni iliyopo Taveta na Holili, Holili, na pale Namanga magari yaweze kutembea, kama suala ni vyeti vya Covid 19 hakuna haja ya mtu wa mataifa haya kupimwa mara mbili. Mawaziri wa afya wajue namna ya kufanya certificate ikitolewa Tanzania iwe sawa na aingie Kenya na vinginevyo,” amesema Rais Kenyata.

 

Awali akiongea kwenye mkutano huo Rais Kenyatta amewataka wawekezaji watanzania kuwa na uhuru kuwekeza nchini Kenya bila kusumbuliwa na masuala ya visa wala vibali vya kazi ila wanao wajibu wa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.

Leave A Reply