The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Atua Zanzibar Kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Tano

0

Rais Magufuli leo Ijumaa Januari 10, 2020 ameanza ziara ya kikazi ya siku tano visiwani Zanzibar. Rais Magufuli  ataweka jiwe la msingi la jengo la Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar.

 

Kesho Jumamosi ya Januari 11 , 2020, Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe iliyopo Mjini Magharibi na atafungua hoteli yenye hadhi ya nyota tano iitwayo Hotel Verde Azam Luxury Resort and Spa iliyopo Mtoni.

 

Rais Magufuli atashiriki Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zitakazofanyika Jumapili Januari 12, 2020 katika uwanja wa Amaan, Mjini Magharibi.

Leave A Reply