The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Awaapisha Mkuu wa Majeshi, Kamishna wa Magereza, Mnadhimu Mkuu na Mabalozi

Rais Magufuliakizungumza baada ya kuwaapisha Mkuu wa Majeshi, Kamishna wa Magereza, Mnadhimu Mkuu na Mabalozi.

DAR ES SALAAM: AMRI Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo amewaapisha Mkuu Mpya wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo kushika wadhifa huo, akichukua nafasi ya Jenerali Davis Mwamunyange aliyestaafu.

Rais Magufuli akimuapisha Mkuu wa Majeshi, Jenerali Mabeyo.

Katika hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ikulu, Rais Magufuli amemuapisha pia Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa na Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali James Mwakibolwa.

Rais Magufuliakizungumza baada ya kuwaapisha Mkuu wa Majeshi, Kamishna wa Magereza, Mnadhimu Mkuu na Mabalozi.

Rais Magufuli pia amewaapisha Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Samwel Shelukindo na Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Paul Meela.

Wakati huohuo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna wa Polisi, Ernest Mangu amemuapisha Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Save

Save

Save

Save

Comments are closed.