The House of Favourite Newspapers

Rais Samia: Mafuta ni Janga la Ulimwengu, Si la Serikali Yamepanda Duniani Kote -Video

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Kata ya Bwanga Wilaya ya Chato Mkoani Geita alipokua njiani akielekea Mkoani Kagera kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu inayoanza tarehe 08 Juni, 2022.

RAIS Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Juni 8, 2022 amezungumza na Wananchi wa Bwanga Wilayani Chato, Mkoani Geita  amesema kwasababu ya Vita inayoendelea Nchini Ukraine, bei ya mafuta imepanda duniani kote

 

Amesema “Bilioni 100 zimetolewa kufidia bei za mafuta zishuke. Mwezi huu bei zimeanza kushuka polepole. Tutaendelea kutoa Ruzuku mpaka duniani kukae sawa. Tutakata Bilioni 100 kila mwezi kwenye matumizi ya Serikali ili kupunguza makali”

 

Ameongeza “Dunia nzima tunaziambia zile Nchi mbili ziache kupigana kwasababu zikiacha, tutapata unafuu wa mambo mengi. Tulikuwa tunaagiza ngano katika mojawapo ya Nchi zinazopigana, sasa haiwezekani. Nchi nyingine mikate ni kwa mgao”

Rais Samia, akisalimiana na Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Geita alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Geita alipokuwa akielekea Mkoani Kagera kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu inayoanza leo Juni 8, 2022.
Rais Samia, akisalimiana na Wasanii wa Vikundi vya ngoma mbalimbali alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Geita, alipokuwa akielekea Mkoani Kagera kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu inayoanza tarehe 08 Juni, 2022.

⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply