The House of Favourite Newspapers

Rais Madagascar Adai Kugundua Dawa Tiba ya Corona

0

WAKATI wanasayansi duniani kote wakihangaika kupata chanjo na tiba ya virusi vya corona, Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina amezindua dawa ya mitishamba ”inayotibu” Covid-19.

 

Hata hivyo Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kuwa hakuna ushahidi wa tiba ya Covid-19 baada ya Bwana Rajoelina kutangaza dawa yake.

 

Taasisi ya taifa ya tiba nchini Madagascar (Anamem) pia imeonyesha wasiwasi wake juu ya ufanisi wa dawa hiyo inayoelezewa na rais Andry Rajoelina kama yenye uwezo wa kuzuwia na kupona corona.

 

 

Taasisi hiyo imesema kuwa mitishamba inaweza kudhuru afya ya mtu kwani “hakuna ushahidi wa ufanisi wake kisayansi”.

 

Mmea huo unatarajiwa kutolewa bure kwa watu wenye uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na na virusi vya corona.

 

Ikizinduliwa kwa jina Covid-Organics, dawa hiyo imetengenezwa kutoka kwa mmea artemisia (pakanga)-ambao ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria.

 

Dawa hiyo ambayo imepakiwa kwenye chupa na kutangazwa kama chai ya miti shamba baada ya kujaribiwa kwa watu chini ya 20 kwa kipindi cha wiki tatu, katibu wa rais Lova Hasinirina Ranoromaro.

Leave A Reply