The House of Favourite Newspapers

Rais wa Zamani wa Sudan Ahukumiwa Jela

0

Aliyekuwa Rais wa zamani wa Sudan, Omary Al Bashir amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, na Mahakama  ya Mjini Kartoum kwa makosa ya kujipatia fedha kwa udanganyifu na matumizi mabaya ya fedha za wafadhili wakati akiwa rais.

Mwishoni mwa mwezi Aprili, mkuu wa Baraza la Kijeshi la Mpito, Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, alidai kwamba Dola sawa na zaidi ya milioni 113 taslimu zilikamatwa katika makazi ya Omar al-Bashir jijini Khartoum.

Mnamo Juni 16, mwendesha mashtaka alisoma mashtaka dhidi ya rais huyo wa zamani, wakati alipoonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu kutimuliwa mamlakani na jeshi Aprili 11.

Leave A Reply