The House of Favourite Newspapers

Rayvanny Aungana na Kiba

0

KAMA ilivyo kwa nguli wa Bongofleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ kuwa na ukaribu wa kipekee na Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho, Msanii mwenzake kutoka lebo ya Next Leval Music, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ naye amejitosa kuwa karibu na Gavana wa Machakos, Alfred Mutua.

 

Magavana hao kutoka nchini Kenya wameonekana kuupenda muziki wa Tanzania kiasi cha kutoa kongole nyingi kwa wasanii wa Bongo.

 

Mbali na Kiba ambaye alianza kuwa karibu na Joho kwa muda mrefu, katika siku za karibuni, Rayvanny ambaye amepikwa katika Lebo ya Wasafi Classic Baby, naye amefuata nyayo za Kiba baada ya Gavana huyo wa Machakos kuweka wazi kuwa anavutiwa sana na kipaji cha msanii huyo.

 

Gavana Mutua ambaye alikuja Tanzania hivi karibuni na kukutana na Rayvanny, tarehe yake ya kuzaliwa ni sawa nay a msanii huyo. Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Mutua alifichua kwamba wamekubaliana kushirikiana na Rayvanny katika kukuza vipaji vya wasanii chipukizi Kenya na Tanzania.

 

Pia gavana huyo alifichua kwamba msanii Rayvanny ana talanta na ni mtu ambaye ni mnyenyekevu. “Nimekuwa na wakati mzuri na Rayvanny msanii mwenye kipaji cha kipekee ambaye alizaliwa huko Mbeya upande wa kusini mwa Tanzania.

 

Rayvanny au Chui na mimi tunashare siku ya kuzaliwa (Agosti 22) na tulitumia alasiri kuimba na kuzungumza juu ya utoto wetu, matarajio na jinsi tunaweza kufanya kazi pamoja ili kuimarisha na kukuza talanta ya muziki wa Afrika Mashariki, alisema.

 

Alisema ingawa Rayvan anatokea katika lebo ya WCB, Rayvanny ana studio yake mwenyewe Next Level Music (NLM) ambayo anatumia kurekodi na kuunga mkono ukuaji wa wasanii wa muziki wa Afrika Mashariki, hasa kutoka Kenya na Tanzania.

 

“Tulikubali kushirikiana katika ubia mchache tunapokuza sanaa. Mimi hivi karibuni nitafunua mpango mpya wa kuwawezesha wasanii wa filamu wenye vipaji na wasanii wa muziki.

 

“Kama mpenzi wa sanaa na mtu anayeamini katika uwezo wa muziki na burudani, ninafurahi kufanya kazi na wasanii wanapoleta nyimbo na vibe kwa maisha yetu. @rayvanny,” alimaliza Mutua.

STORI; MWANDISHI WETU

 

 

Leave A Reply