The House of Favourite Newspapers

Recho: Kama ni Rahisi Nao Wakadange

0

MREMBO mwenye sauti nyororo kwenye Bongo Fleva, Winfrida Josephat au Recho Kizunguzungu amevunja ukimya baada ya kuambiwa anategemea kudanga ili aendeshe maisha yake.

Akistorisha na IJUMAA SHOWBIZ, Recho ambaye mwenye matashtiti ya aina yake anasema kuwa, walimwengu huwa hawakosi jambo la kumsema mtu sasa kama wanaona kudanga ni rahisi na wao wakajaribu.

“Eti nadanga, jamani kama ni rahisi, basi na wao wakadange, halafu tuone kama watapendeza kama mimi, walimwengu wameshazoea kuongea na mimi siwezi kuwazuia kusema kwa sababu binafsi najua namna ambavyo naendesha maisha yangu,” anasema Recho ambaye amekuwa akilalamikiwa kwamba hasikiki kulingana na kipaji kikubwa alichonacho.

STORI; MEMORISE RICHARD, DAR

Leave A Reply