The House of Favourite Newspapers

Riek Machar Aondoka Sudan Kusini

0

machar-new

Dkt. Riek Machar.

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini, Dkt Riek Machar, ameondoka nchini humo wiki chache baada ya mapigano makali kuzuka kati ya vikosi vyake na wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kiir huko mjini Juba.

Msemaji wa Machar, James Gatdet Diak amesema kiongozi huyo amefanikiwa kuhamia taifa jirani, ambalo hakulitaja jina lake.

Salva-Kiir

Rais Salva Kiir.

Rais Kiir alimfuta kazi Dkt Machar mwezi uliopita na nafasi yake kuchukuiwa na Bw Taban Deng Gai.

Dkt. Machar awali alisema hatarejea Juba hadi kuwepo na kikosi cha wanajeshi wasioegemea upande wowote cha kumlinda.

Leave A Reply