The House of Favourite Newspapers

Roma, Stamina Wakabidhi Ventilator, Mashuka Hospitali Morogoro – Video

0

MOJA Stori zilizogusa mioyo ya Watanzania leo Alhamisi, Mei 20, 2021 ni kuhusu wasanii wa kizazi kipya (bongo fleva) Roma Mkatoliki na Stamina wanaounda Kundi la ROSTAM wametoa msaada wa ventilator (mashine ya kusaidia kupumua) na mashuka 33 katika hospital ya Mkoa wa Morogoro.

 

Kwa niaba ya kundi hilo msanii Stamina amesema walichangisha fedha kutoka kwa wadau wao kusaidia upatikanaji wa vifaa hivyo ili kuokoa maisha ya watu wengi ambao wanapata shida ya upumuaji hasa watoto wadogo wanaozaliwa wakiwa njiti.

 

Pia, ventilator hizo zitasaidia hata watu wazima na kwa kuanza wameanzia katika mkoa wa Morogoro na wataenda Tanga kupeleka na kuwataka watu wengine kujitolea zaidi vifaa katika hospital kwani bado vinaitajika zaidi.

 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospital ya mkoa wa Morogoro, Dokta Nkungu Daniel amesema kupokea kwa vifaa hivyo vitasaidia kupunguza vifo mabavyo vinatokana na upungufu wa vifaa hasa kwa watoto wadogo na vifaa hivyo watavipeleka katika wodi ya watoto iwasaidie zaidi.

 

Aidha, mmoja wa mama ambaye anauguza mwanaye hospital hapo amewashukuru wasani hao kwa kujitolea vifaa hivyo na kuwaomba waendelee kutoa zaidi kwa wenye wahitaji.

 

Leave A Reply