The House of Favourite Newspapers

Ronaldo akataa bilioni 4 kwa wiki China

ronaldoMadrid, Hispania

IMEFAHAMIKA kuwa staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo alikuwa ana nafasi ya kuweka rekodi ya kulipwa mshahara mkubwa zaidi duniani katika wachezaji wa soka kama angekubali ofa ya kwenda kucheza nchini China.

Wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes amesema kuna klabu ilikuwa tayari kumlipa Ronaldo pauni milioni 1.6 (Sh bilioni 4.1) kwa wiki kisha kutoa ada ya usajili pauni milioni 260 ili kumsajili.

Kwa kiwango hicho, ina maana Ronaldo ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Ballon d’Or 2016 ndiye ambaye angekuwa mchezaji anayepokea mshahara mkubwa akimzidi hata Carlos Tevez aliyejiunga na Shanghai Shenhua na mshahara wake unatajwa kuwa ni pauni 615,000 kwa wiki.

“Wachina walikuwa tayari kumsajili kwa pauni milioni 260 na kumlipa mshahara wa pauni milioni 85 kwa mwaka lakini fedha siyo kila kitu,” alisema Mendez.

“China kuna soko jipya la soka, wanaweza kusajili wachezaji wengi lakini hawawezi kumsajili Ronaldo,” alisema Mendes.

Jarida la Forbes lilitoa takwimu hivi karibuni kuwa, ukijumuisha mishahara na maingizo yote ya fedha ambayo Ronaldo anaingiza kwa mwaka inaaminika yanafika pauni milioni 71.

WACHEZAJI WANAOLIPWA ZAIDI KWA WIKI

1. Tevez (Shanghai Shenhua) Pauni 615,000
2. Oscar (Shanghai SIPG) Pauni 400,000
3. Ronaldo (Real Madrid) Pauni 365,000
4. Messi (Barcelona) Pauni 365,000
5. Bale (Real Madrid) Pauni 346,000

Comments are closed.