The House of Favourite Newspapers

Rosa Ree Amfungulia Kesi Harmonize

0


MSANII wa muziki Bongo, Rosa Ree, amefunguka kuwa kesi yake dhidi ya msanii Harmonize kwa sasa ipo kwenye mikono ya sheria ikiangaliwa ni jinsi gani haki inaweza kutumika kwa sababu muziki ni biashara.

 

Rosa Ree amesema wimbo wake wa Kanyor Aleng aliwahi kumsikilizisha Harmonize awali lakini akashangaa kuja kusikia kitu kinachofanana na hicho.

 

Julai 26, mwaka huu wimbo wa Harmonize unaokwenda kwa jina la Amen uliondolewa kwenye mtandao wa YouTube kutokana na wimbo huo kufanana mdundo na wimbo wa Rosa Ree uitwao Kanyor Aleng.

 

Harmonize alitoa wimbo huo (Amen) kufuatia kifo cha Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ambao  umeelezea mazuri kibao yaliyofanywa na  Mkapa enzi za uhai wake na jinsi dunia ilivyobaki na simanzi kwa kuondoka kwake.

 

Hii ni mara ya pili kutokea kwa Harmonize kutokewa na kadhia kama hii ambapo mwanzo ni kwenye wimbo wake wa  Uno ambao ilisemekana una vionjo vya mdundo wa Prodyuza kutokea Kenya, Magix Enga.

Leave A Reply