The House of Favourite Newspapers

Rose Muhando ‘Afufuka’, Afanya Kweli

0

 

DAR: Mwanamuziki mkali wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando ‘amefufuka’ na kufanya kweli kwenye tamasha lililokwenda kwa jina la Pamoja.

Tamasha hilo lilifanyika mjini Nakuru nchini Kenya wakati wa mkesha wa Mwaka Mpya wa 2020.

Rose ambaye nyimbo zake zimekuwa zikigusa hisia za wengi kwa miaka na miaka, alisisimua umati wa mamia ya watu waliohudhuria kwenye tamasha hilo ambao walikuwa wakimshangilia na kucheza naye mwanzo hadi mwisho.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya, katika tamasha hilo, Rose ameacha historia ya aina yake na kwamba wengi hawakutarajia kama angeburudisha kiasi hicho.

Wakenya walioshuhudia tamasha hilo hawakuchelewa kuonesha upendo wao huku wakijaa kwenye mitandao ya kijamii kumpongeza na jumbe mbalimbali za kumtia moyo. Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 44 aliwagusa zaidi Wakenya alipokuwa akiimba Wimbo wa Mungu Ilinde Kenya ambapo alionesha mapenzi makubwa kwa nchi hiyo, hivyo kuwa na mashabiki wengi nchini humo.

Mbali na Rose, wengine waliotumbuiza kwenye tamasha hilo ni Upendo Nkone, Emmy Kosgei, Pastor Musembi, Solomon Mkubwa, Guardian Angel na wengine wengi.

Stori: MWANDISHI WETU, Ijumaa

Leave A Reply