The House of Favourite Newspapers

Rose Muhando Amlaani Mchungaji

0

MWIMBA Injili maarufu Bongo, Rose Muhando anadai kukosa utulivu baada ya kukosolewa vikali na mwimbaji wa zamani wa nyimbo za Injili nchini Kenya ambaye kwa sasa ni mchungaji aitwaye Mr T Mwangi.

Rose Muhando anadai kukewa na kauli ya mchungaji huyo wakati wa ibada hivi karibuni.

 

Rose Muhando ameposti video ya mchungaji huyo akitumia jina lake kama mfano wakati wa ibada. Katika video aliyoposti Rose Muhando kwenye ukurasa wake wa mtandao wa TikTok, mchungaji huyo anaoneshwa akiwa kwenye madhabahuni akimkosoa vikali mwimbaji huyo kwa kuingia katika mkataba na Lebo ya Sony Music.

 

Mchungaji huyo anasema Rose Muhando amekuwa akijaribu kurejea kwenye ulingo wa muziki wa Injili, lakini imekuwa vigumu kwani watu wengi ikiwemo yeye binafsi hawamtambui.

 

“Amejaribu kurudi, lakini imeshindikana, amepitia kila aina ya maombi ya kumfungua, lakini hakuna kitu. Alikuwa ameanzisha ufufuo wa muziki Tanzania, akasaini mkataba na Sony Records akanyamaza,” anasema mchungaji huyo.

 

Mchungaji huyo anasema Rose Muhando alidhania kuwa hatua hiyo itasaidia muziki wake, lakini ilikuwa sivyo kwani ilichangia kuporomoka kwake.

Anasema kuwa, alikuwa anashauri kondoo wake dhidi ya kutokuwa wepesi wa kuingia katika dili zote zinazojitokeza.

 

Kwa upande wake, Rose Muhando ameeleza kukerwa na matamshi hayo akisema yalilenga kumdhalilisha huku akisema anatakiwa kulaaniwa kwa kutumia matamshi hayo makali dhidi yake.

“Huyu pasta na alaaniwe, ameninena vibaya sana,” amesema Rose Muhando.

 

Leave A Reply