The House of Favourite Newspapers

Ugomvi wa Kiba, Shilole Wasambaa Kama Moto wa kifuu

0

TASNIA ya Bongo Fleva inazidi kupasuka kadiri muda unavyosonga, kisa ni ugomvi wa wasanii King Kiba na Shilole ambao umeendelea kusambaa kama moto wa kifuu.

 

Baada ya Kiba kudai kwamba hakumualika Shilole kwenye listening party ya albam yake hivi karibuni na kwamba alishangaa kumuona, kumeendelea kuibuka mambo mengi na sasa mpasuko umekuwa wa wazi zaidi.

 

Mwanzoni, baadhi ya wasanii wakubwa hawakutaka kujitokeza hadharani kutoa maoni yao juu ya suala hilo, lakini sasa kila mmoja anasema waziwazi kwamba yupo upande gani.

 

Kwa sasa, mastaa wengi ama wapo upande wa Kiba au Shilole pamoja na kwamba wengine hawataki kusema waziwazi.

 

Hata hivyo, watu wa karibu wa wasanii hao wanadai kwamba, ugomvi wa Kiba na Silole ni zao la ugomvi wa Kiba na Diamond Platnumz.

 

Kundi linalomuunga mkono Shilole akiwemo yeye mwenyewe ni lile lililopo nyuma ya Diamond na ndiyo wanaoongoza kumshambulia Kiba.

 

Wasanii kama Gigy Money, Amber Lulu, Baba Levo na wengine wamekuwa wakimshambulia Kiba kwamba, amemshindwa Diamond na sasa amehamia kwa wanawake.

 

Kwa upande wake, Kiba anaungwa mkono na wasanii wengi, lakini ambao wanajionesha waziwazi ni pamoja na Snura, Esha Buheti na wengine.

 

Leave A Reply