The House of Favourite Newspapers

Rose Ndauka: Naapa sitazaa tena nje ya ndoa!

0

rose_ndauka_2012Mwanadada anayeuza nyago kwenye filamu Bongo, Rose Ndauka.

MAYASA MARIWATA
MWANADADA anayeuza nyago kwenye filamu Bongo, Rose Ndauka ameapa kuwa sasa hivi atajitahidi sana kuhakikisha hazai tena nje ya ndoa kwani anajua amemkosea Mungu na ndugu zake pia.

Akipiga stori na paparazi wetu, Rose alisema anajua alifanya kosa kujiachia na kubeba mimba nje ya ndoa lakini sasa amejifunza na hawezi kurudia kosa hilo.

“Sasa hivi niko makini kuliko mnavyofikiria, najizuia sana kuhakikisha sizai tena kabla ya kuingia kwenye ndoa. Yaani nitakuwa ni mwenye amani endapo mtoto wangu wa pili nitamzaa nikiwa ni mke wa mtu, Mungu anisaidie katika hilo,” alisema Rose.

Leave A Reply