The House of Favourite Newspapers

RWANDA 0-0 TANZANIA ‘LIVE’ FULL TIME, KUFUZU CHAN 2018

0

FULL TIME

Dakika ya 90 +3: Mwamuzi anamaliza mchezo. Mtokeo ni 0-0, Taifa Stars inaondolewa kwenye mbio za kuwania kufuzu kucheza CHAN, Rwanda inasonga mbele hatua inayofuata.

Dakika ya 90 + 2: Bado presha ni kubwa kutoka kwa pande zote mbili zinazoshambuliana kwa zamu.

Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.

Dakika ya 89: Stars wanapanda mbele kwa kupiga pasi ndefu kutafuta bao lakini Rwanda wapo makini kuzuia.

Dakika ya 86: Stars nao wanashindwa kutumia vizuri nafasi ya wazi wanayopata, shambulizi lao linatoka nje.

Dakika ya 85: Kasi ya mchezo inaongezeka, Stars wanapambana kutafuta bao lakini bado mambo ni magumu.

Dakika ya 82: Rwanda wanapata nafasi ya wazi kabisa wanashindwa kuitumia vizuri, shuti linatoka nje kidogo ya lango baada ya uzembe wa walinzi wa Stars.

Dakika ya 82: Mchezo unachezwa zaidi katikati ya uwanja.

Dakika ya 80: Taifa Stars wanapata kona, inapigwa wanashindwa kuitumia vizuri, kipa wa Rwanda anadaka.

Dakika ya 78: Mchezo unaendelea kwa kasi na inavyoonekana wenyeki wakipata bao moja tu wanaweza kuupoozesha zaidi.

Dakika ya 73: Wachezaji wa Rwanda wanaanza kuonekana kupoteza muda.

Dakika ya 70: Kiungo wa Rwanda anamchezea faulo nahodha wa Stars, Himid Mao nje ya eneo la 18, inakuwa faulo, anapiga Nyoni lakini walinzi wanaokoa.

Dakika ya 67: Kasi ya mchezo imeongezeka, wenyeji ndiyo wanaotafuta bao kwa nguvu, matokeo yakibaki hivi Rwanda itafanikiwa kusonga hatua inayofuata na Tanzania itakuwa imetolewa.

Dakika ya 63: Rwanda wameongeza kasi na wanalishambulia lango la Stars kwa nguvu.

Dakika ya 58: Rwanda wanapata faulo nje ya eneo la 18, wanapiga lakini walinzi wa Stars wanaokoa.

Dakika ya 50: Matokeo bado ni 0-0

Kipindi cha pili kimeanza.

Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili.

MAPUMZIKO

Kipindi cha kwanza kimekamilika matokeo ni 0-0. Timu zote zimeingia vyumbani kupumzika.

Dakika ya 20: Mchezo umeanza kubalansi, timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dakika ya 5: Taifa Stars ndiyo ambayo imekuwa na kasi kubwa katika kushambulia.

Mchezo umeanza.

Mchezo huu ni wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji Wachezaji Wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN), katika mchezo wa kwanza timu hizo zilimaliza kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Leave A Reply