The House of Favourite Newspapers

Sababu 7 za Chelsea Kumsajili Coutinho

0

MSIMU huu wa 2019/20 umekuwa wa kupanda na kushuka kwa Chelsea, kuna wakati unawaona kama ‘wanakuja hivi mara wanakataa’, chini ya kocha wao moyo, Frank Lampard mambo yamekuwa siyo mazuri kwa kiwango cha juu.

Chelsea inaundwa na vijana wengi, kuna kitu wanakikosa na inavyoonekana wameshindwa kuziba pengo la aliyekuwa staa wa timu yao, Eden Hazard.

 

Msimu uliopita timu hiyo ilikuwa haina mastaa wengi, hivyo mzigo mkubwa ukaonekana kumuelemea Hazard, alilifanya kweli na kuiwezesha kubeba taji la Europa League.Msimu huu ni mara nyingi Lampard amesikika akitamka maneno ya ‘fi ziki’ na ‘ubunifu’, bila shaka hivyo ni vitu vikubwa viwili ambavyo kikosi chake inavikosa.

 

Lampard amekuwa ni mtu ambaye anaonekana ana muono wa mbali na kuna vitu ametengeneza kwenye timu yake lakini bado kiuhalisia mambo hayajawa kwenye ubora kama wengi walivyotegemea.

Kinachomkwamisha kingine ni kwenye suala la ushambuliaji na kutengeneza mashambulizi. Tangu Hazard aondoke ni wazi kuna vitu vimekosekana kwenye safu hizo mbili yaani ya kufunga na ile ya kutengeneza mashambulizi.Unazibaje pengo la mtu aliyekuwa na ubora wa juu kama Hazard?

 

Ni swali gumu, hilo ndilo ambalo linawatesa kwa sasa, hadi ligi zinasimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona, imeonekana wazi kuwa kuna kitu kinatakiwa kifanyike ili kuifanya timu hiyo kuwa bora zaidi ya ilivyo sasa, na hapo ni msimu ujao.

 

Hivi hapa ni baadhi ya sababu ambazo zinatajwa kuwa zinaweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa timu hiyo kuamua kumsajili kiungo mshambuliaji wa Barcelona, Phillipe Coutinho.Kabla ya kuzisoma sababu hizo ikumbukwe kuwa Coutinho ni mmoja wa wachezaji bora duniani katika nafasi yake, alipokuwa Inter Milan alikuwa bado chipukizi, ukomavu wake na ustaa mkubwa aliupata akiwa Liverpool.

 

Moto aliouwasha Liverpool ulimfanya awe nyota wa timu na kuiweka timu hiyo begani kwake, kujiamini, ufundi, uwezo wa kufunga, akili ya haraka kukawafanya Barcelona wamsajili lakini bahati mbaya mambo hayakuwa kama vile LONDON, EnglandHivi hapa ni baadhi ya sababu ambazo ikumbukwe kuwa Coutinho ni mmoja wa wachezaji bora duniani katika nafasi yake, alipokuwa Inter Milan alikuwa bado chipukizi, ukomavu wake na ustaa mkubwa Moto aliouwasha Liverpool ulimfanya ambavyo wengi walitegemea iwe.

 

Licha ya kucheza katika kikosi bora cha Barcelona huku staa wa timu hiyo, Lionel Messi akijaribu kumsaidia kuzoea mazingira mara kwa mara bado imeshindwa kumsaidia.

 

Akatolewa kwa mkopo Beyern Munich ambako amekuwa mzuri lakini dalili za kununuliwa jumla nazo zinaonekana kukwama kwa kile ambacho Barcelona wanakitaka kama ada ya usajili.Barcelona walimsajili kwa ada ya pauni milioni 105, kwa sasa umri wake ni miaka 27, hivyo wanaona kushindwa kung’ara kwake siyo ‘ishu’, anaweza kufanikiwa kwingine na bado umri unamruhusu, hiyo inawafanya watake dau kubwa ili kufi dia gharama zao za usajili na pili wanaamini bado ni Mbrazili huyo ni mchezaji wa kiwango cha juu zinatajwa kuwa zinaweza Barcelona, Phillipe Coutinho.ambao kwa sasa wametawala katika kikosi cha kwanza cha Chelsea.

 

Coutinho ameshacheza mechi nyingi za Ligi ya Mabingwa Ulaya, na kwa hatua hiyo anaweza kuwa ni msaada mkubwa kwenye kikosi cha Chelsea.

 

UMAARUFU WA JINA NI FAIDA

Kumsajili mchezaji kama Coutinho kuna faida kubwa kibiashara, mfano kama kwenye mauzo ya jezi, kuvutia mashabiki wengi uwanjani na kwenye biashara nyingine mbalimbali zinazoweza kutumia jina lake klabu kuneemeka.

 

Mbali na hayo pia inaonyesha jinsi gani klabu ilivyo na nguvu na inavyoweza kuwa na ushawishi wa kusajili wachezaji wakubwa, hiyo itasaidia katika mradi huu wa sasa wanaoufanya wa kutengeneza timu yao kurejea kwenye mbio za mataji baada ya kuyumba kwa muda.

 

Mbali na hapo mashabiki watakuwa na furaha na inaweza kuwa sehemu ya kuongeza morali ya timu na klabu katika kujiona nao ni wakubwa na thamani yao ipo juu.Kwani kuna wachezaji wengi ambao wamekuwa wakifeli wanapotua kwenye Premier League kwa kuwa inatajwa kuwa ni aina ya ligi ambayo inahusisha nguvu nyingi na kasi.

YUPO KWENYE UMRI SAHIHI

Ana umri wa miaka 27, kwa hapo alipo ni umri sahihi wa mwanasoka kuwa amekomaa na anayejua afanye nini hasa kama ameshapita kwenye mikiki ya hapa na pale.Kwa aina ya chakula wanachotumia wachezaji wa sasa, ubora wa masuala ya afya kwa umri wake anaweza kuendelea kucheza kwa miaka mitano zaidi akiwa na ubora wa juu tangu umri alionao sasa hivi.

 

Ikiwa Chelsea watamsajili na kufanikiwa kupata kile kilicho bora kutaka kwake, inamaanisha kuwa watakuwa wamevuna zao zuri ambalo watalitumia kwa mufa mrefu kujineemesha.Uzoefu wake unaweza kuwa sehemu nzuri ya kuwapa hamasa wachezaji vijana wanapotua kwenye Premier League kwa kuwa inatajwa kuwa ni aina ya ligi ambayo inahusisha nguvu nyingi na kasi.

 

YUPO KWENYE UMRI SAHIHI

Ana umri wa miaka 27, kwa hapo alipo ni umri sahihi wa mwanasoka kuwa amekomaa na anayejua afanye nini hasa kama ameshapita kwenye mikiki ya hapa na pale.Kwa aina ya chakula wanachotumia wachezaji wa sasa, ubora wa masuala ya afya kwa umri wake anaweza kuendelea kucheza kwa miaka mitano zaidi akiwa na ubora wa juu tangu umri alionao sasa hivi.Ikiwa Chelsea watamsajili na kufanikiwa kupata kile kilicho bora kutaka kwake, inamaanisha kuwa watakuwa wamevuna zao zuri ambalo watalitumia kwa mufa mrefu

ADA YA KUMUUZA NI SAHIHI

Inawezekana Chelsea wakamchukua kwa mkopo pia au wa kuamua kumsajili moja kwa moja, yote mawili yanawezekana. Ikiwa Barcelona wataamua kumuuza moja kwa moja ni vizuri pia kwa kuwa wanajua wakifanya hivyo watapunguza matumizi ya mishahara wanaomlipa huku akiwa hana faida kubwa kwenye timu.Chelsea wanaweza kuzungumza nao vizuri ili wamsajili kwa pauni 60m au chini ya pauni 80m kwa kuwa kiwango hicho ni pungufu ya kile kilichotumiwa na Barcelona kumsajili wakati akitokea Liverpool mwaka 2018.

MUDA SAHIHI

Chelsea wana nafasi nzuri ya kumsajili Coutinho kwa kuwa mwenyewe ni kama ameshaonyesha nia ya kutaka kurejea England na kucheza katika Premier League.

 

Barcelona nayo imeonyesha nia ya kutaka kumuuza yaani kinachokwamisha ni kuwa halijapatikana dili la uhakika tu la kumsajili. Hivyo, hiyo inaweza kuwa nafasi nzuri kwa Frank Lampard ambaye enzi zake alikuwa bora kwenye nafasi kama ya Coutinho kujua anaweza vipi kumtumia Mbrazili huyo, muda wake wa kufanya maamuzi ni huu kwa kuwa kila kitu kipo kwenye wakati wake.

 

ANAUJUA MCHEZO

Hadi ligi zinazimama Coutinho alikuwa amefunga mabao tisa akiwa Bayern Munich msimu huu, hiyo inaonyesha bado ana kitu mguu.Alicheza Liverpool kwa miaka mitano, akawa staa mkubwa na mwenye mafanikio uwanjani, hiyo inamaanisha anaujua mchezo na anajua aina ya ligi ambayo anaweza kucheza akiwa Chelsea.Coutinho anaonekana ni kama mlaini fl ani hivi lakini anapokuwa na mpira ni mchezaji mwenye nguvu, anajua wapi apige pasi na wakati gani, hizo ni sifa ambazo zinaweza kuwa na msaada mkubwa kwa Chelsea.

 

KUTHIBISHA UBORA WAKE

Hii inawezekana ikawa nafasi ya mwisho kwa Coutinho kutaka kuthibitisha kwa ulimwengu kuwa bado ana uwezo wa juu na anaweza kuwa staa mkubwa duniani.Kuyumba kwake akiwa Barcelona kunaweza kuchangia kushusha thamani yake, kitendo cha Liverpool pia kutotaka kumrejea klabuni hapo lazima kitakuwa kimemuuma, hivyo ni nafasi yake kuonyesha ulimwengu kuwa bado anaweza.Kusajili kwa mkopo kwenda Bayern Munich kutamfanya awe na hasira ya kumrejesha Coutinho yuleee aliyefanya Barcelona ikavunja akaunti na kutoa dau nono katika kumsajili.

 

KUBORESHA THAMANI YA KIKOSI

Kule juu tuliona jinsi ambavyo Lampard anayataja maneno mawili likiwemo ‘ubunifu’, Coutinho anaweza kuondoa msongo wa mawazo wa kocha huyo kwa kumpatia kile anachoona kimekosekana kwenye kikosi chake.Katika suala la ubunifu ni wazi kuwa anajua nini anachokifanya, anaweza akawa hana kasi kama Hazard lakini kwenye ubunifu na kuibeba timu wakawa wanaendana.Hivyo, Chelsea inaweza kutazama usajili huu kwa jicho chanya kama hili na kuamua kujivika mabomu ikiamini imepata jembe kwenye usajili huu ambao wanasoka wengi ni kama wana hofu juu ya Coutinho kwa sasa.

Leave A Reply