The House of Favourite Newspapers

Sakata la Gigy Money, Eric Omondi Akamatwa na Polisi

0

Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi Filamu nchini Kenya (KFCB), Dkt Ezekiel Mutua, ametangaza kwamba mchekeshaji Eric Omondi, amekamatwa kwa kukiuka kanuni ya maadili ya bodi hiyo.

 

 

”Maafisa wa Ufuatiliaji wa Bodi ya Uainishaji wa Filamu Kenya wakishirikiana na Maofisa wa Polisi kutoka Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) jana mchana wamemkamata Eric Omondi kwa kukiuka masharti ya Sheria ya Filamu na Maonyesho ya Sura 222 ya Sheria za Kenya kwa kutengeneza na kusambaza filamu ambayo haijaidhinishwa kwa jinataarifa ya Dkt. Mutua ilisema.

 

 

Kama hatua ya kutia mkazo tangazo hilo Dkt. Mutua pia ameweka tangazo hilo katika Twitter yake. Hii sio mara ya kwanza Dkt Mutua na Eric Omondi kutofautiana kuhusu maudhui ya filamu hiyo.

 

Katika onyesho jipya la filamu hiyo, “Wife Material” wa Eric Omondi inayojumuisha wahusika kutoka Kenya na Tanzania wanaonekana wakipigana hadharani na kulazimu polisi kuingilia kati.

 

 

”Vita hivyo” vilianza wakati mmoja wa warembo hao aliangusha meza na kuvunja glesi zilizokuwa mezani na kumwaga vileo.

 

 

Kanda ya filamu hiyo iliyosambazwa mitandaoni imeibua mjadala mkali baadhi ya mashabiki wake wakiuliza ikiwa ni uigizaji au ni uhalisia. Hatua hiyo imemghadhabisha Mkuu wa KFCB, Ezekiel Mutua, aliyetaja kuwa filamu “iliyooza.”

 

 

Aidha Bw. Mutua amesema Bodi itachukua hatua zote zinazowezekana za kisheria kuzuia utengenezaji na maonyesho ya filamu zisizoruhusiwa kwenye jukwaa lolote linalokusudiwa kuwa maonyesho ya umma.

 

Leave A Reply