The House of Favourite Newspapers

Afungwa Siku Moja kwa Kumuua Mume Wake

0

MAHAKAMA nchini Kenya imemhukumu kifungo cha siku moja mwanamke aliyemuua mume wake mwaka mmoja uliopita, Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation. Jaji Roselyn Aburili alimpata Truphena Ndong’a Aswani na kosa la kumuua mumewe Disemba 14, mwaka jana.

 

 

”Hakua na sauti. Alinyamazishwa kwa kichapo hadi akakubali kupigwa ni jambo la kawaida. Ana bahati yuko hai”, gazeti hilo lilinukuu maneno aliyotumia Jaji Aburuli.

 

 

Mtuhumiwa alionewa huruma na Jaji kwa kuvumilia mateso na kumhukumu kifungo cha siku moja ambacho hakikujumuisha kuzuiliwa ndani.

 

 

Aidha Jaji Aburili aliagiza idara ya mahakama kuhakikisha Bi Truphena amepewa usafiri wa kwenda hadi nyumbani kwake Ukwala katika Kaunti ya Siaya Magharibi mwa Kenya.

 

 

Ni nini kilitokea?

Bi Truphena aliye na umri wa miaka 49 aliifahamisha mahakama kwamba alivumilia mateso katika ndoa yake ili kumtunza mwanawe wa kiume na watoto wengine wanne walioachwa na mama zao (wake wa awali) wa Bw. James Oyengo Obochi.

 

 

Siku ya mkasa, mahakama ilifahamishwa Bw. Obochi alirejea nyumbani usiku akiwa mlevi kama ilivyo ada akapewa chakula. Baada ya kula huku akiwa amelewa alianza kuzozana na mkewe akidai kupewa hati miliki ya shamba la familia.

 

 

Alipokataa kumpatia nyaraka hizo kwa kuhofia anaweza kuzitumia kuuza shamba lao, alikimbilia chumbani na kuchukua panga kumkata mke wake. Lakini alimshinda nguvu katika purukushani hilo akamuua katika juhudi za kujilinda.

Leave A Reply