The House of Favourite Newspapers

Sallam Afungukia Wasanii vs Management

0
MENEJA wa Supastaa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Sallam Ahmed Sharaff maarufu kama Sallam Sk au Mendez atatua utata wa kile kinachodaiwa kuwa chanzo cha muziki wa Bongo fleva kuzalisha wasanii wengi wenye vipaji vikubwa wasio na mafanikio yeyote kimuziki.
 
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter, ambapo Sallam Sk amebainisha wazi anachokiona kuwa tatizo namba moja kwa wanamuziki wengi wa Tanzania kutofanikiwa kufika sehemu ya ndoto zao licha ya kubarikiwa talanta za hali ya juu.
 
“Tanzania kuna wasanii wengi wazuri tu, kuna uhaba wa management inayojua muziki, elimu kwa wasanii kujua umuhimu wa management, na sheria inayomlinda investor, muhimu kabisa kila mtu kujua jukumu lake na maamuzi yawe ya team sio ya mtu mmoja!!,” ameandika Sallam.
Leave A Reply