The House of Favourite Newspapers

Tunamtakia Kila la Heri Mbwana Samatta Kwenye Utoaji tuzo leo Nigeria

0

gfMbwana Samatta

Muda huu tunahesabu saa chache kuelekea tukio la utoaji wa Tuzo za Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mwaka 2015 lifanyike huko Abuja, Nigeria.

Mwakilishi wa Tanzania kwenye tuzo hizo ni Mbwana Samatta ambaye anawania Tuzo za Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mwaka 2015 kwa upande wa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

Mbwana ametumia nafasi hii kuwashukuru Watanzania na ametumia akaunti yake ya Instagram kwa kuandika hivi: “Nafurahi kwa support mnayonionesha Watanzania. Nina imani mmeniombea kwa Mungu kiasi cha kutosha. Najivunia kuwa Mtanzania na haitajalisha matokeo ya tuzo bali kwa ukarimu wenu. Asanteni”

sama

Leave A Reply