The House of Favourite Newspapers

Samia: Sina Ujuzi wa Kuhesabu Matofali na Mabati Kama Magufuli – Video

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Magufuli alihesabu matofali na maati kujua ubadhirifu katika miradi ya Serikali lakini yeye hawezi, badala yake anawategemea wateule wake kubaini ubadhirifu.

 

Samia amesema hayo leo Jumatano, Juni 2, 2021 wakati akiwaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa na viongozi mbalimbali aliyowateua hivi karibuni, katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

 

“Nimewasimamisha wakuu wa mikoa na Ma-RAS ili nione, kama umesoma Sociology utagundua huko kutakuwa na nini, ndio maana nilipomsimamisha RC Mwanza na RAS nikaona hiki ni kiberiti na petroli, Ngusa ni mkimya yule kule ni mlipukaji, sijui itakuwaje ila sisi tutaangalia.

 

“Kuna tuliowabadilisha vituo, si kwamba mlitenda mabaya mlikotoka, kubadilika ndio kukuza uzoefu na kujifunza zaidi, ukizoea palepale hutafanya vizuri, ukienda sehemu mpya nenda na mazuri acha mabaya kule, kafanye kazi.

 

“Wengine hawakuwa kwenye uongozi, tumewaibua, kaonyesheni kwamba mnaweza kufanya kazi. Nimepata malalamiko mbona huyu alikuwa balozi ameshushwa, hapana, RAS ni dhamana kubwa, tunaamini mtakuwa washauri na wasimamizi wazuri.

 

 “Nendeni mkasimamie matumizi mazuri ya serikali, Hayati Dkt. Magufuli, alikuwa na huo ujuzi wa kwenda na kuhesabu mabati na matofali, lakini mimi sina huo ujuzi mimi ujuzi wangu ni grafu za uchumi si ujuzi wa construction engineering, nyie mtanisaidia huko.

 

“Nimelaumiwa sana nilipomteua Batlida kwamba huyu alikuwa Balozi kwanini kamshusha, hukushushwa u-RAS ni dhamana kubwa nenda kafanye kazi kuna matarajio mengi wananchi wanatusubiri.

 

“Kamanda Wambura umefanya kazi nzuri sana, utumishi wako katika Jeshi la polisi ni wa kutukuka, hivi karibuni tulikuwa na changamoto Dar es Salaam umefanya kazi nzuri sana na ndicho kilichonivutia nikuweke hapo sasa kuwa DCI,” amesema Rais Samia.

 

Leave A Reply