The House of Favourite Newspapers

Serikali Yakumbushwa Ahadi ya Ujenzi wa Wodi ya Wagonjwa Kituo cha Afya Nyamatongo

0

Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo ya afya Nyamatongo kilichopo wilayani Sengerema Mkoa Mwanza, Stivin Godwin ameiomba serikali kutimiza ahadi ya ujenzi wa wodi za wangonjwa kwenye kituo hicho iliyotolewa na Waziri wa afya Ummy Mwalimu  alipotembelea kituo hicho miaka ya nyuma.

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 2, 2023 mwaka huu alipokuwa akisoma taarifa ya kituo hicho mbele ya kamati Tekelezaji ya umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza ilipokuwa ikikagua utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye Kata ya Nyamatongo.

Amesema Kituo hicho kwa sasa kinahudumia wagonjwa 900 hadi 1000 kwa mwezi huku kwa siku kinahudumia wagonjwa 30 hadi 50 na kinatoa huduma kwa magojwa mbalimbali likiwemo tatizo la ugonjwa wa moyo.

Kituo cha afya Nyamatongo kinaendeshwa na Serikali kwa ubia na Shirika lisilo la kiserikali la Cedar Foundation.

Godwini amesema wanapata changamoto kubwa wanapopata wagonjwa wanaopaswa kulazwa huku kituo hicho kikiwa na sehemu ya kupumuzisha akina mama ambao wamemalaza kujifungua na wangonjwa wengine wa dharula hivyo wodi zinahitajika ili wananchi waweze kupata huduma stahiki.

” Kituoa afya Nyamatongo kinahudumia Kata nne za Nyamatongo, Ngoma Chifunfu na Katunguru hivyo wagonjwa wanaotoka mbali wanahangaika kutokana na kutokuwa na wodi, amesema Godwin.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Sengerema, Patrick Mundeba amewatoa hofu watumishi wa Kituo cha afya Nyamatongo kuwa ahadi zote zilizotolewa na Serikali kwenye kituo hicho zitatekelezwa .

Wao kama UVCCM wanatawasilisha ngazi za juu ili ahadi  iliyotolewa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ya Ujenzi wa Wodi za wangojwa kwenye kituo hicho iweze kutekelezwa na wananchi waweze kupata huduma.

Sambamba na hilo amewamwagia sifa wa watumishi wa Afya wa Kituo hicho kwa kutoa huduma bora kwa wangojwa ambao wanafika katika kituo hicho kupata huduma za afya.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati Tekelezaji wa UVCCM Wilaya ya Sengerema, Paul Mfumakule amewaomba wananchi wanaopata changamoto ya afya waendee kituo cha afya Nyamatongo kutokana na huduma bora zinazotokewa na watumishi wa Kituo hicho.

Baadhi ya wangojwa waliokuwa wakipatiwa huduma ya matibabu kwenye kituo hicho cha Afya Nyamatongo wamewashukuru wajumbe wa Kamati Tekelezaji ya UVCCM Wilaya ya Sengerema kwa kuwatembea kisha kuwajulia hali na kuchukuwa changamoto za ukosefu wa wodi za wagonjwa kwenye kituo hicho.

Kamati Tekelezaji wa umoja wa Vijana UVCCM Wilaya ya Sengerema ikiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Patrick Mundeba wamefanya ziara ya kwenye Kata ya Nyamatongo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye nyanja ya Elimu, na afya ambapo wameipongeza Serikali kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa sambamba na kituo cha afya Nyamatongo.

Leave A Reply