The House of Favourite Newspapers

Shahidi Akwamisha Kesi ya Idris Sultan – Video

0

Kesi ya kutumia laini ya simu ambayo haijasajiliwa kwa jina lake inayomkabili msanii wa vichekesho nchini, Idris Sultan imepigwa kalenda Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Yusto Ruboroga hadi Januari 26, 2021 baada ya shahidi aliyetarajia kutoa ushahidi kutokuwepo mahakamani.

 

Idris anakabiliwa na shitaka la kushindwa kusajili laini ya simu iliyokuwa ikitumiwa na mtu mwingine. Mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara Innocent Maiga anayekabiliwa na kosa la kushindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya umiliki wa laini ya simu hiyo.

 

Washitakiwa hao kwa pamoja awali wakisomewa hati ya mashtaka waliyakana mashitaka yao, isipokuwa majina yao na anwani zao ambapo wanatetewa na wakili Jebra Kambole.

 

Leave A Reply