The House of Favourite Newspapers

Shilole Aporomosha Matusi Hadharani!

Zuwena Mohammed ‘Shilole’ akiwa jukwaani.

Na MUSSA MATEJA| IJUMAA WIKIENDA| HABARI

DAR ES SALAAM: Hakika neno aibu yake ndilo sahihi unapotaka kuelezea madudu yaliyofanywa na staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ au ‘Shishi Trump’ baada ya kujikuta akiporomosha matusi mazito hadharani, mbaya zaidi mbele ya wageni waalikwa.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na Wikienda ambalo lilisababisha watu kupigwa na butwaa, lilijiri wakati Shishi akitumbuiza kwenye jukwaa la shoo ya uzinduzi wa Malkia wa Nguvu uliofanyika katika Ukumbi wa High Sprit, Posta jijini Dar, usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.

Akiwa ukumbini hapo kabla ya kuanza makamuzi ya shoo hiyo, Shishi alionekana akiwa ameketi peke yake kwa utulivu wa hali ya juu tofauti na alivyo siku zote.

Baadaye utulivu huo ulitafsiriwa kuwa inawezekana alikuwa na stresi kwani baada ya kutakiwa akatumbuize tu, alicharuka ghafla. Alipopanda stejini, kabla ya kuimba, alianza kwa kujinadi kwa kuongea kimombo ‘yai’ akatumbuiza wimbo wake wa Say My Name kisha ukafuatiwa na Sitoi Kiki ambapo baada ya kumaliza kuimba wimbo huo alimtaka DJ, aache kupiga muziki kisha akaanza tena
kujinadi juu ya umalkia wake wa nguvu.

Shishi alisema yeye ni mjasirimali wa kuuza chakula na kwamba anamshukuru sana Mungu kwa kuendelea kumjalia neema ya kupata wateja kila kukicha hivyo akawataka na wasichana wenzake wasichague kazi za kufanya na badala yake wajikite kwenye fursa ambazo wengi wanazionea aibu wakati ndizo zenye masilahi.

Wakati akiongea hayo, ghafla mazungumzo yaliingia kirusi hivyo alijikuta akipandisha mori na kuanza kuongea Kiingereza kisha akaporomosha matusi ya nguoni mbele ya umati wa wageni waalikwa ambao wengi walikuwa wanawake watafutaji.

Alipofutwa na gazeti hili na kuulizwa kulikoni, Shishi alishtuka na kuuliza kama ilikuwa ni ishu, alipoambiwa ni ishu, aliomba Mungu isisambae mitandaoni.

“Kwani nimeharibu? Kwani kuna mtu amechukua video? Naomba Mungu isiingie mitandaoni,” alisema Shishi aliyeonekana ‘kuchangamka’.

 

Comments are closed.