The House of Favourite Newspapers

Shilole: Ray Alikuwa Mteja Wangu, Nilimwambia Mi’ Mzuri Kuliko Uwoya

0

STAA wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ au ‘Shishibaby’ ametoboa siri namna ambavyo alisaidiwa na msanii wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ wakati akimtambulisha kwenye tasnia ya filamu na kumfanya kuwa maarufu.

 

Shilole ameanika hayo jana Jumatano, Agosti 12, 2020, usiku wakati akifanya mahojiano na Clouds TV kuzungumzia maisha yake na namna alivyopambana mpaka kufika hapo alipo leo.

 

“Ray Kigosi alikuwa mteja wangu alikuwa anakuja sana kwenye mgahawa niliokuwa nafanya kazi, nilimzoea sana na kila alipokuwa anakuja nilikuwa namhudumia vizuri, nakumbukua alikuwa anapenda kula samaki Sato nilikuwa namchagulia samaki mkubwa.

 

“Kuna siku siku nilimpigia simu nikamwambia nataka kuigiza, na kuwa mimi ni mzuri kuliko Irene Uwoya, akaniambia niende ofisini kwake Sinza, nilichukua bajaj nikawakuta yupo na Johari na Uwoya waliniambia niigize namtongoza Ray, siku ile ile walinirekodi scene.

 

“Tangu nikiwa kijijini Igunga moyo wangu ulikuwa unaniambia ipo siku utakuwa maarufu, utapesa pesa, utakuwa na biashara zako, utaenda nchi za nje lakini hutafanya yote haya ukiwa hapa, ndiyo maana nikatoka Igunga kuja Dar,” amesema Shilole.

 

Leave A Reply