The House of Favourite Newspapers

Shilole, Uchebe Hapatoshi

0

BAADA ya penzi lao kufi kia ukingoni kwa maneno mengi, mwanamama anayekiwasha kwenye Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ na aliyekuwa mumewe wa ndoa, Ashraf Uchebe, hali ni tete kiasi kwamba, sasa hapatoshi mjini.

 

Kila mmoja amekuwa ‘akimfokea’ mwenzake kwa vijembe na mbwembwe kama zote mitandaoni, huku wakioneshana umwamba wa nani zaidi.

 

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, limefanya exclusive interview (mahojiano maalum) na Uchebe, ambapo kwa upande wake, amesema kuwa, ameshaamua kuendelea na maisha yake (move-on), hivyo sasa hivi hana muda tena wa kumkumbuka zilipendwa wake huyo.

IJUMAA WIKIENDA: Mambo vipi Uchebe?

Uchebe: Poapoa, niambie?

IJUMAA WIKIENDA: Safi tu, naona upo bize na kazi zako za kutengeneza magari…

Uchebe: Ndiyo, si unajua tena, lazima maisha mengine yaendelee…

IJUMAA WIKIENDA: Sawa kabisa, hivi zile picha za Shilole akiwa na mpigapicha wake huwa hazikuumizi?

Uchebe: (Anacheka) kwa nini ziniumize wakati sasa hivi nina maisha yangu ninayoyafurahia, nipo bize sana, halafu huwa nikiachana na mtu, ninamsahau mazima.

IJUMAA WIKIENDA: Hivi vile vijembe ukiwa na ‘chombo’ kipya, ulikuwa unamuwekea nani mtandaoni?

UCHEBE: Vijembe gani?

IJUMAA WIKIENDA: Si vile, mara ooh mwanaume kifua, kwani mpenzi wa Shilole hana kifua?

Uchebe: Unajua raha ya mwanaume ni kifua, lazima uwe na kifua ili mpenzi wako apate sehemu ya kuegemea, halafu mimi kuandika vile, haina maana kwamba nimemsema mtu.

IJUMAA WIKIENDA: Unayazungumziaje mapenzi mapya ya Shilole?

UCHEBE: Siwezi kumuongelea mtu ambaye sipo naye kwa sasa.

IJUMAA WIKIENDA: Kuna tetesi kwamba, unataka kumuoa yule mpenzi wako unayemposti kwenye akaunti yako ya Instagram.

Je, ni kweli? Uchebe: Mimi ni mtoto wa kiume, siwezi kukaa muda mrefu bila kuwa na mwanamke, halafu wewe mwenyewe si unaona jinsi pisi ilivyo kali ile, hayo mambo mengine uliyoyasikia kuhusu ndoa, tuendelee kusubiri, huwenda ikawa kweli.

 

Baada ya kumaliza kuzungumza na Uchebe, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilimtafuta Shilole, ambaye naye kwa upande wake, alisema hawezi kurudiana na Uchebe kwa sababu alipo kwa sasa anapata amani ya moyo.

IJUMAA WIKIENDA: Shishi baby…

SHILOLE: Ndiye mimi…

IJUMAA WIKIENDA: Hebu tuweke wazi kidogo kuhusu uhusiano wako na huyo mpigapicha, maana hatuwaelewi?

SHILOLE: Msichokielewa ni nini hapo?

IJUMAA WIKIENDA: Zile picha zenu za kimahaba, ndizo zinaleta sintofahamu kwa mashabiki, wengi wanasema kuwa tayari ninyi ni wapenzi…

SHILOLE: Mimi yule ni mpigapicha wangu, ninampenda sana kwa sababu ananiheshimu, anaediti picha zangu, zinakuwa nzuri, anafanya kazi kwa wakati, yaani ananijali na kunithamini, sasa kuna ubaya gani nikimpenda?

IJUMAA WIKIENDA: Vipi unazungumziaje uhusiano mpya wa Uchebe?

SHILOLE: Wewe mimi siwezi kumzungumzia mwanaume ambaye nimemlea mwenyewe, hebu niache.

 

TUJIKUMBUSHE

Shilole na Uchebe walifunga ndoa ya Kiislam na kuishi pamoja kwa takribani miaka minne kabla ya penzi lao kuingia doa, ambapo waliachana, huku Shilole akidai kupokea kipigo kizito na kumpeleka jamaa huyo mahakamani.

Baada ya kuachana, kila mmoja amekuwa bize na maisha yake, ambapo inasemekana kwa sasa, mwanamama huyo anatoka kimapenzi na mpigapicha wake aitwaye Rommy3d huku Uchebe naye akibanjuka juu kiaina na mrembo anayejulikana kwa jina la Agness Suleiman.

Tetesi zilizoshika vichwa vya habari wiki hii ni kwamba, Uchebe na Agness wapo mbioni kuoana na kuwa mke na mume.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Leave A Reply