The House of Favourite Newspapers

Sifa kwa TGNP: Kikundi cha Sauti ya Jamii Kipunguni Chazindua Mradi wa Kuchakata Mkaa

0
Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi (kulia) akizungumza kwenye mkutano huo.

 

 

KIKUNDI cha Sauti ya Jamii cha Kipunguni jijini Dar, kilichopo kati ya vikundi vya taarifa na maarifa vilivyopo chini ya Mtandao wa Jinsia (TGNP) kimezindua mradi wa kuchakata mkaa mbadala baada ya kuwezeshwa na shirika la kimataifa la Amref.

Katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto  ambapo pia kulikuwa na wageni wengine wa heshima akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi, Meneja wa SIDO mkoa wa Dar, Ridhiwani Matange, Diwani wa Kata ya Kipunguni Danny Malagashimba na wengineo ambapo wote kwa pamoja walishiriki katika uzinduzi huo.

Sehemu ya umati uliofurika kwenye hafla hiyo ukimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi.

 

 

Akizungumza kabla ya uzinduzi huo Mkurugenzi wa kikundi hicho, Selemani Bishagazi amesema mafanikio ya mradi huo yametokana na kuchukuliwa na TGNP na kwenda kupewa mafunzo ya Nishati Jadidifu namna ya kutengeneza mkaa mbadala yaliyokuwa yakiwezeshwa na Amref.

Bishagazi amesema baada ya kupata mafunzo hayo walitembelea vikundi vya wenzao ambavyo vilishaanza uchakataji wa mkaa huo na kujifunza kwa vitendo zaidi.

Mkurugenzi wa kikundi hicho, Selemani Bishagazi akizungumza kwenye hafla hiyo.

 

 

Ameendelea kusema kuwa baada ya kupata mafunzo na kwenda kujionea kwa vitendo nao waliweza kupata elimu kamili hivyo nao wakaanza kuwafundisha wenzao maeneo ya mtaani kwao.

Hapo ndipo wakaanza kujipiga picha wakiwa kwenye kuwafundisha wenzao kuchakata mkaa huo na kuzipost TGNP, Amref na kwa wadau wengine.

Kutokana umahiri waliouonesha kwenye kutoa mafunzo hayo kwa jamii Amref iliwaona kupitia posti zao na kuwakubali hivyo kuwawezesha mradi huo na kupata mashine ya kuchakata mkaa huo na kuwajengea sehemu ya kukaushia taka wanazotumia.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto akizungumza kwenye hafla hiyo.

 

 

Bishagazi kwa niaba ya kikundi hicho wameishukuru TGNP kwa kuwapa mafunzo mbalimbali na kuwaunganisha na Amref ambapo sasa mradi huo unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 30 na hivyo kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira haswa kwa vijana waliozagaa mitaani na kufanya kazi zisizo rasmi.

 

Baada ya shukrani hizo kwa TGNP kutoka kwa mkurugenzi wa kikundi hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi naye alipata nafasi ya kuzungumza ambapo alisema;

 

“Siku ya leo ni ya kipekee sana kwa jamii ya Kipunguni na TGNP ambao ni walezi wa vituo vya taarifa na maarifa ambavyo vipo zaidi ya sabini hapa nchini na vimeshawafikia watu zaidi ya milioni tano.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP akimpongeza Mwenyekiti wa Kikundi cha Sauti ya Jamii Kipunguni, Fatma Abdulrahman baada ya kutunuwa cheti na SIDO kufuatia mafanikio ya mradi huo.

 

 

 

“Nipende kusema kama mzazi anavyofurahia mafanikio ya mtoto wake ndivyo nasi tunavyofurahia mafanikio ya kikundi hiki leo kikiwa zao la TGNP.

 

“Sisi kama TGNP tumewafundisha vitu mbalimbali kama vile jinsi ya kutandaa, kutafuta marafiki na mbinu mbalimbali za kujikwamua kimaisha.

 

Pamoja na hayo tumewawezesha kukutambua haki na wajibu wa viongozi wao hivyo niwape pongezi sana kikundi cha Sauti ya Jamii Kipunguni ambapo mara nyingi sana mmekuwa mkiibua na kutatua changamoto mbalimbali za maeneo haya, mmekuwa tegemeo letu kubwa sana kwa maeneo haya ya Kipunguni,” alimaliza kusema Mkurugenzi Lilian wa TGNP.

 

Baada ya Mkurugenzi Lilian, Mgeni rasmi katika hafla hiyo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto alianza na kukipongeza kikundi hicho baada ya kukagua miradi yake ambapo kabla ya kwenda kuzindua uchakataji wa mkaa huo alianza kukagua miraji ya kikundi hicho ambapo alianza kuoneshwa darasa ya wanafunzi waliokuwa wakifundishwa ushonaji.

 

Baada ya kukagua darasa hilo ndipo alienda kufanya uzinduzi rasmi wa mradi huo wa kuchataka mkaa mbadala uliowezeshwa nashirika la Amref.

 

Meya Kumbilamoto alikisifu kikundi hicho na kueleza jinsi alivyoguswa na shughuli wanazozifanya na kusema kwamba mradi huo wa kuzifanya taka kuwa mkaa utasaidia kutunza mazingira na kuongeza kuwa suala la mazingira litamgusa mpaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ambaye hata yeye aliwahi kufanya kazi katika ofisi inayohusika na mazingira kabla ya kuwa Rais.

 

Meya Kumbilamoto aliwaomba wanakikundi hao kuutunza mradi huo ili uendelee kutoa ajira na kuokoa gharama za uzoaji wa taka ambapo sasa hakutakuwa na gharama ya kuwapa taka wazoaji wa taka wanaokwenda kuzitupa dampo.

HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply