The House of Favourite Newspapers

Siku zote mke, mama mkwe ni maadui

0

LOVE3.jpgNIANZE kwa kuwashukuru wasomaji wangu kwa kuendelea kufuatilia mada zangu mbalimbali za Maisha na Uhusiano na hata kutoa maoni na ushauri. Asanteni sana.

Mke na mama mkwe hawa ni wanawake wawili toka koo mbili tofauti, mmoja akiwa ni muolewaji na mwingine ni mama wa muoaji na wanaunganishwa na tendo la binti kuolewa na kijana wa mama husika. Hii ndiyo mada yangu ya leo; siku zote mke, mama mkwe ni maadui!

Niende moja kwa moja kwenye mada hii, nilichojifunza katika maisha haya siku zote hawa watu wawili ni maadui wa asili ingawa si wote. Narudia tena, ingawa si wote!

MSINGI WA MADA

Msingi mkubwa wa mada ya leo nataka kuweka wazi baadhi ya tabia zinazofanywa na akina mama wakwe  mpaka kufikia hatua ya kuharibu ndoa za watoto wao wa kiume.

Kwa kweli inashangaza sana, unatengeneza mazingira ya kuharibu ndoa ya kijana wako na mkewe ili ufaidike na nini?

SIYO WOTE

Yawezekana mke wa mwanao (mwinga) akawa kweli ana matatizo lakini pia hata wewe mama mkwe waweza kuwa ni tatizo, tena tatizo haswaa!

Migongano na mipishano katika familia ni jambo la kawaida sana na kama ndivyo sioni kama kuna mantiki ya kufikia hatua ya kuharibu ndoa ya mtoto wako, hata kama mwinga wako kakukorofisha sana!

UTAVUNJA NDOA NGAPI?

Hivi kweli kwa makwazo yetu binadamu kama wewe mama kila ukikorofishwa au ukiudhiwa na mke wa kijana wako unafanya mpango wa kumuachananisha, utavunja ndoa ngapi za kijana huyo? Na mwisho wa yote siyo wewe utakayeonekana ni tatizo pekee hata huyo mwanao.

HISIA ZA KUMTAMANI MWANAYE

Ndiyo maana kuna wengine hufika mbali zaidi kimawazo kwa kufikiria labda mama mkwe anakuwa anamtaka au anamtamani mtoto wake wa kiume. Wapo wanaofika mbali kiasi hicho. Sasa wasemeje na wao ni binadamu?

Utakuta mama anafanya kila namna ili awe na uhuru na mwanae kwa kumtazama au kuwa naye karibu muda wote, hilo ni tatizo kubwa. Mawazo ni mengi yanayoweza kusemwa na kufikiriwa kwa mama mwenye tabia kama hii.

USHUHUDA MEZANI

Najaribu kukupa ushuhuda wa mkasa wa kweli wa binti (jina kapuni) wa miaka 27 ambaye ndoa yake imevunjika miezi mitatu iliyopita kisa kikiwa ni mama mkwe. Tena kisa chenyewe ni cha kijinga na kisichoeleweka.

MIAKA 4 YA UCHUMBA, NDOA?

Binti alidumu kwenye uhusiano na kijana wa mama huyo kwa miaka 4 kabla ya ndoa.

Baada ya uhusiano wa miaka mingine 4 walikubaliana kufunga ndoa ili wawe huru na amani zaidi katika uhusiano wao.

Usikose sehemu ya ushuhuda huu wa ukweli katika toleo lijalo.

Leave A Reply