The House of Favourite Newspapers

Sinema ya Husna Sajenti ‘Kuzaa’ na Mondi Yafikia Patamu!

0

IKIWA ni wiki kadhaa zimepita tangu kuwepo kwa tetesi kuwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amezaa na aliyekuwa Miss Sinza mwaka 2011, Husna Maulid hatimaye sinema yao imezidi kunoga na kuwafanya watu kuzidi kuamini kwamba huenda ni kweli.

 

ISHU ILIVYOKUWA

Juni 21, mwaka huu mrembo huyo ambaye pia aliwahi kushiriki Miss Tanzania 2011, aliposti picha ya Diamond kwenye akaunti yake ya Instagram na kumtakia heri ya siku ya kina baba duniani, ambapo baadhi ya mashabiki walimjia juu na kusema kuwa anajipendekeza na kutafuta kiki.

 

“Kwani wewe huna baba au huyo mtoto wako hana baba? Au Mondi ndio baba yake? Kwa nini wasichana mnapenda kujidhalilisha hivi?” alikomenti shabiki mmoja aliyefahamika kwa jina la @Aneth.

 

MTANDAONI KWACHAFUKA

Haikushia hapo kwani huko mtandaoni hali iliendelea kuwa mbaya huku kila mmoja akisema lake, wapo waliompongeza kwa kuzaa na msanii huyo kwa maana ya kwamba mtoto wake atapata matunzo lakini wapo pia waliomuonea huruma na kusema ataachwa solemba kama walivyoachwa wanawake wengine wa Mondi.

 

HUSNA AZUNGUMZA

Hata hivyo, baada ya mambo kuwa mengi mtandaoni mwanamama huyo alifanyiwa mahojiano na baadhi ya vyombo vya habari ili afunguke ukweli wa mtoto wake kama ni wa Diamond au lah na baada ya kujua ana mimba yake alijisikiaje, ambapo aliishia kucheka na kusema anafurahi kwa sababu anahisi mtoto wake atakuja kuishi vizuri hapo baadae.

 

MONDI ACHARUKA

Wakati mambo yakiendelea kutaradadi, Mondi aliibuka na kuposti ujumbe mrefu kwenye akaunti yake kuwa anawaheshimu sana wanawake lakini hicho kisiwe kigezo cha wao kusema mambo ambayo hayana ukweli.“Nashukuru sana kwa upendo mkubwa wa madada mbalimbali ambao unazaidi kuongezeka siku hadi siku juu yangu, nawathamini na nawapenda zaidi.

 

“Ila tafadhali kama unajua hatujawahi na wala hatuna mahusiano ya kimapenzi usiseme tuna mahusiano maana inakuwa haikai vyema na pia kibinadamu si sawa kwa mimi sasa hivi nianze kumtoa mtu nishai mtandaoni, nawapenda sana na nashukuru kwa sapoti kubwa mnayonipa,” aliandika Diamond katika ukurasa wake kupitia kipengele cha Insta Story huku watu wakidai ujumbe huo ulimlenga Husna.

 

HUSNA AJIBU

Mara baada ya msanii huyo kuposti maneno hayo, mrembo huyo naye hakukaa kimya alimjibu kwa kusema: “Nacheka lakini naogopa, eti tukukome.” Kama hiyo haitoshi, Husna akaongeza: “Inashangaza watu wanavyoamini uongo wa huyu mwanaume lakini ukweli upo wazi.

 

”Baada ya kuona mambo yamezidi kuwa mengi, RISASI lilimvutia waya mwanamama huyo ili kutaka kujua ukweli wa jambo hilo.Mlimbwende huyo baada ya kupatikana alisema, anashangaa kuona mtu anapingana na ukweli.

 

“Unajua watu wanaongea sana tena wanaongea vitu wasivyovijua kiundani vipoje, mimi nawaangalia tu lakini ukweli upo na ipo siku utajulikana, nimeona huo ujumbe wa Mondi na kama unavyojua mtu akishawaza kitu fulani huwezi kubadilisha tena mawazo yake, pia siwezi kusema kama tumewahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi au hatujawahi kila kitu kina muda wake,” alisema Husna.

Leave A Reply