The House of Favourite Newspapers

Sababu Tanasha Kutoenda Msiba wa Shammy

0

HIVI karibuni yameibuka mazito yakimhusisha mzazi mwenza wa mwanamuziki mkubwa barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Mondi’, Tanasha Donna, kutohudhuria msiba wa mke wa mmoja wa mameneja wa Wasafi, Hamis Taletale ‘Babu Tale’, Shamsa Kombo ‘Shammy’.

Baada ya kifo cha Shammy, watu mbalimbali wenye ukaribu na jamii ya Wasafi iliyo chini ya Mondi, walifika msibani kuanzia Dar hadi kule Morogoro, lakini Tanasha.

Lakini wakati Tanasha akijadiliwa, hali tofauti kwa mzazi mwenza mwingine wa Mondi, Hamisa Mobeto ambaye alikuwa amejaa tele msibani kama pishi la mchele.

Tanasha alipata habari za msiba kuposti kwenye ukurasa wake wa Instagram kutoa pole kwa Babu Tale, kutokana na kumpoteza mkewe Shammy.

Baada ya kufanya hivyo, mashabiki wakaibuka na kusema kuwa, Tanasha ameogopa maneno ya Wabongo.

“Sababu kubwa ya Tanasha kutoenda msibani na kuishia kuposti, ni kwa sababu ameogopa kusemwa kuwa anajipendekeza tu,’’ alidokeza mtu wa karibu wa Tanasha.

STORI:HAPPYNESS MASUNGA, DAR

Leave A Reply