The House of Favourite Newspapers

Siri ya Bill Nass na Sugu Yafichuka

0

RAPA maarufu Bongo, William Nicholaus Lyimo Bill Nass amefunguka chanzo cha ukaribu wake na legend wa muziki huo wa rap nchini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na kusema mkongwe huyo ni miongoni mwa wasanii ambao wamechangia yeye kuwa msanii.

Nenga amesema; “Nimekuwa shabiki mkubwa wa muziki wa bongo fleva kabla ya kuwa mwanamuziki, nimekuwa nikifuatilia na kusikiliza kazi za wasanii mbalimbali waasisi ndio imenijenga mimi kuwa mwanamuziki kwa sababu nilianza kupenda na kukariri nyimbo za watu.

 

“Sugu ni moja kati ya wasanii ambao nawapenda na ninaheshimu mchango wao kwenye sanaa kwa sababu wasingekuepo watu kama hao labda mimi nisingefanya hichi ninachokifanya. Huwa naheshimu kile alichokifanya napenda kazi zake na zipo nyingi zilizokuwa zikinibamba ni kaka na nimekuwa nikisapoti vitu vyake vingi.

 

“Wakati yupo jela nilienda kumuona kama brother kama msanii mwenzangu hatukua na ukaribu lakini mwenyewe alishangaa nilivyoenda kumuona kwa sababu najua ni maisha ambayo yanaweza kumkuta mtu yoyote, kwa hiyo kuanzia pale akawa ni brother ambaye tunawea kusalimiana vizuri,” amesema Bill Nass.

Leave A Reply