The House of Favourite Newspapers

Siri ya Mondi, Tiffah Yaanikwa

0

MSANII Nasibu Abdul ‘Diamond’ au Mondi kuwa karibu zaidi na mwanaye Tiffah kuliko Nillan kuna jambo limejificha, Risasi Jumamosi limedokezwa siri.

Tangu watoto wa msanii huyo aliyezaa na Zarinah Hassan ‘Zari’ raia wa Uganda kutua Bongo wakitokea Afrika Kusini walipokuwa wakiishi na mama yao, Mondi amekuwa ‘klozi’ na Tiffah huku Nillan akionekana kuwa na ukaribu zaidi na mama yake.

MAMBO YALIANZA HIVI:

“Mi sielewi haya mapichapicha ninayoyaona, kwa nini Diamond hapendi kuwa karibu na Nillan.

“Kila mara anaonekana akiwa na Tiffah au mzee kuna jambo linamsumbua?” msichana mmoja alihoji mtandaoni baada ya picha za Mondi akiwa amembeba Tiffah kusambaa.

Aidha, mjadala kwenye mitandao wa kijamii ulikuwa mkubwa baada ya picha nyingi kuletwa jamvini na ‘wafuatilia ya watu’ na kuonesha kuwa nyingi kati ya hizo zilionesha Mondi akiwa na Tiffah na Zari akijiachia kwa upendo mkubwa na Nillan.

TUTAFUTE MAJIBU

Kufuatia mjadala huo kufika mbali, Risasi Jumamosi lilimtafuta kwa njia ya simu Daniel Omondi mkazi wa Nairobi nchini Kenya ambaye ni mtaalam wa masuala ya malezi na saikolojia ya ukuaji wa mtoto na kumuuliza hali hiyo inayojitokeza kati ya Zari na Mondi kimalezi imekaaje?

“Mara nyingi mtoto hupitia hatua za msingi kama tano hivi katika makuzi yake, hatua ya kwanza huitwa Oral Stage, hatua hii huwahusu watoto wa kuanzia siku moja mpaka miaka miwili ambapo furaha ya mtoto hutawaliwa zaidi na mdomo mfano kunyonya maziwa ya mama yake na kunyonya vidole.

“Anal stage ni hatua ya pili ambayo humhusu mtoto wa miaka miwili au mitatu. Kwenye hata hii mambo yanayohusu matumizi ya mwili huwa yanajitokeza sana mfano kupendelea kutumia sehemu zake za haja kwa kukojoa au kwenda haja kubwa mara kwa mara.

“Ya tatu ni Phallic Stage, hii inawahusu watoto wa wenye umri wa miaka minne na kuendelea kidogo.

“Hatua ya nne ni Latency Stage, hatua hii huwahusu watoto wa miaka sita hadi miaka 12 ambapo katika hatua hii watoto hutawaliwa zaidi na michezo ya kawaida.

“Hatua ya mwisho inaitwa; Genital Stage, hii ni hatua muhimu sana na mara nyingi huwahusu watoto wa kuanzia miaka 13.

“Kimsingi hatua hii ndiyo mjenzi mkuu wa maisha ya mtoto na mara nyingi mtoto huzirejea hatua nyingine zote nne alizopitia, kama mtoto alipita kwenye hatua za awali vizuri basi hatua hii akiongozwa vizuri ni rahisi kwake kuivuka salama.

“Katika hatua hii ndiyo vijana wengi huanza kubalehe na kuvunja ungo,” alisema Omondi.

SIRI UKARIBU WA TIFFAH, MONDI NI HII

Baada ya kueleza hatua hizo tano za ukuaji wa mtoto, mtaalam Omondi anasema wazazi wanatakiwa kufahamu mchanganuo wa tabia hizi kwa kina na kuongeza kuwa kilichopo kati ya Mondi na mwanaye ni masuala ya kisaikolojia zaidi.

“Sasa kwa kuwa umeniuliza kitaalam ukaribu wao umekaaje; mimi naweza kukurejesha kwenye hatua ya tatu ya makuzi ya mtoto ambayo ni ya msingi kabisa.

“Kumbuka kuwa katika kipindi hiki ndipo mtoto huanza kutambua jinsia yake na hapo huamua kuchagua mzazi wa kuwa naye karibu.

“Mara nyingi mtoto wa kiume hupenda kuwa karibu na mama yake na mtoto wa kike hupenda kuwa karibu na baba yake.

“Hali hii hutokea yenyewe na kujenga hali ya furaha kati ya mzazi wa kike kuwa karibu na mwanaye wa kiume na mzazi wa kiume kuwa karibu na mwanaye wa kike, kitaalam hali hii huitwa ‘Interest of opposite sex’.

“Wakati fulani mtoto wa kiume huweza kumchukia baba yake bila kujua, wataalam wanasema kichocheo kikubwa cha chuki huwa ni wivu.

“Ni kama mtoto wa kike huwa hapendi mama yake apewe mapenzi na baba yake na hivyo kuamua kuziba mwanya kwa yeye kutaka kuwa karibu zaidi na baba yake na mtoto wa kiume humuona baba yake kama anafaidi upendo kwa mama yake na hivyo kuitwaa nafasi hiyo ili upendo na raha apate yeye,” alisema na kuongeza:

“Umewahi kukuta msichana yuko kwenye kundi la wanaume halafu haogopi chochote? Ukifuatilia utakuta mtoto huyu hakupata ukaribu wa baba yake na hivyo anairudia hiyo tabia ya kujifungamanisha na wanaume, sasa kitamtokea nini huko hilo ni jambo jingine.

“Lakini huu ndiyo msingi wa ukaribu wa watoto wa kike kwa baba zao na kwa kumalizia tu watoto wengi wa kiume huwa wanapenda kuoa wanawake ambao wanafanana tabia na mama zao ndiyo maana wazazi wanatakiwa kuwa makini sana na malezi ya watoto ili kutowaathiri kisaikolojia.”

STORI:

MWANDISHI WETU

Leave A Reply