The House of Favourite Newspapers

IGP SIRRO: HII NDO GARI ILIYOMTEKA MO, ILIPOTELEA KAWE – VIDEO

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama limefanya uchunguzi wa tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji na kufuatilia CCTV Camera zilizonasa tukio hilo.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Sirro amesema baada ya gari kutoka Colosseum liliingia kwenye Barabara ya Ally Hassan Mwinyi kuelekea ’round about’ ya kwenda Kawe, tunafuatilia kama walienda Silver au Kawe na kwamba gari hilo lilitokea nchi jilani na kuingia hapa Tanzania Septemba 1, 2018.

 

“Tumepata details za kutosha, nani mwenye gari nchi anayotoka imefahamika, watu wetu wa Interpol wanafanyia kazi. Picha za gari nitawapa muweze kuzisambaza, gari lenyewe ni aina ya Toyota Surf yenye namba ya usajili AGX 404 MC. Hatuwezi kusema kama Mo yupo hai au la kwa sababu sisi sio watekaji, na kufahamu sababu ya kutekwa kwa mfanyabishara huyo, hadi hapo tutakapompata yeye na watekaji.

 

“Tunashirikiana vizuri na ‘Interpol’ bado hatujaona haja ya kuomba msaada wa vyombo vya uchunguzi kutoka nje, kama tutaona kuna ulazima sisi tutamshauri Amiri Jeshi Mkuu, lakini mpaka sasa bado tuna imani na vyombo vyetu vya ndani.

 

“Tusidharau vitisho, mtu unapoona unatishiwa na mtu yeyote, tupe taarifa, ili tuweze kufanyia kazi mapema. Na pia wale wenye uwezo kifedha ni vyema wakawa na silaha na wasaidizi wenye silaha, kwa sababu fedha walizonazo kila mtu anazitaka.

 

“Mo anamiliki silaha lakini siku hiyo hakuwa na silaha, ana dereva lakini siku hiyo aliendesha gari mwenyewe. Kuna vitu unaweza viachia sababu ukijua nchi yetu ni shwari halafu watu wabaya wakachukua hiyo nafasi.

 

“Naomba tupeane taarifa za ukweli, taarifa sahihi na si taarifa za majungu. Ninapokea taarifa nyingi, unaambiwa Mo Dewji yupo sehemu flani mnatumia mbwa na magari lakini hamkuti kitu, hii kwa sababu mtu anadhani anaweza kubahatisha akapata fedha,” alisema Sirro.

MSIKIE SIRRO AKIONYESHA GARI HILO HAPA

Comments are closed.