The House of Favourite Newspapers

Skendo Baab’kubwa za Mastaa 2019

0

 

MAISHA ya mastaa hubebwa na mambo mengi. Yapo ya kuburudisha, kuelimisha na mengine yatakuacha mdomo wazi.

Kuna vitimbi na vituko! Kubwa zaidi ni skendo za kila kukicha. Gazeti la IJUMAA linakuletea skendo baab’kubwa za mastaa zilizotikisa Bongo kwa mwaka 2019;

 

WEMA

Namba moja kama kawaida ilikwenda kwa staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu aliingia mwaka 2019 akiwa amebeba skendo aliyovuka nayo kutoka mwaka 2018. Ni ile ya kuvuja kwa picha na video zake chafu akiwa kimahaba na yule jamaa aliyemtambulisha kwa ‘future husband’, Patrick Christopher ‘PCK’.

 

Wema alijikuta akipambana na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar. Kesi hiyo ilisababisha Wema kulala korokoroni kwenye Gereza la Segerea jijini dar kwa muda wa wiki mbili. Msala huo uliisha baada ya Wema kulipa faini ya shilingi milioni mbili.

 

AMBER RUTY

Video vixen, Amber Ruty hakuwa nyuma kwenye orodha hii. Amber Ruty ‘alitrendi’ baada ya kusambaa kwa video yake akiwa mtupu na kusema ni pombe ndizo zilimsababishia yote.

Ikumbukwe kuwa Amber Ruty alikuwa tayari ana kesi mahakamani kufuatia kuvuja kwa video zake zikimuonesha akiingiliwa kinyume na maumbile na mpenzi wake, Saidi Mtopali.

Hata hivyo, mwaka huu haukuisha salama kwani hivi karibuni aliachana na jamaa huyo.

 

SISTER FAY

Namba tatu ilikwenda kwa Sister Fay ambaye ilivuja video yake akiwa mtupu bafuni hivyo kuitwa kwenye Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwenda kujieleza ambapo alipewa onyo kali kisha kuahidi kubadilika.

 

SANCHI

Mwanamitindo Sanchi naye hakubaki salama kwani ilivuja video iliyodaiwa ni ya kwake akiwa mtupu na lile umbo lake matata. Kwenye ishu hiyo, Sanchi aliibuka na kukanusha kuwa video hiyo haikuwa yake na pia Basata walimkana kuwa siyo msanii aliyesajiliwa kwenye baraza hilo.

 

MENINAH

Namba tano ilikwenda kwa msanii Meninah ambaye video yake akiingiliwa ilivuja mitandaoni huku watu wakitumiana kwenye makundi ya WhatsApp.

Skendo hiyo ilimhusisha mwigizaji Mwijaku ambaye alidaiwa ndiye aliyeivujisha. Hata hivyo, Meninah aliitwa Basata kisha kulazimika kuomba radhi huku uchunguzi wa ishu hiyo ukiendelea.

 

EBITOKE

Mwingine anayeingia kwenye orodha hii ni mchekeshaji Ebitoke ambaye alikuwa ni mpenzi wa mwigizaji, Yusuf Mlela.

Ebitoke alimvamia Mlela hotelini na kumfanyia vurugu akidai kumsaliti na kwenda kwa mwanamke mwingine aliyetajwa kwa jina la Stella au Beyonce.

 

UWOYA

Ukiachilia mbali ishu ya kudaiwa kuwa, kuna video yake ya utupu ambayo ilisababisha tafrani mjini ambapo kila mtu alikuwa akiomba kupata ‘koneksheni’, skendo nyingine ni ile ya kuwarushia waandishi pesa kama mtu anayerushia mbwa chakula iliyosababisha kunangwa kila kona.

 

Kama hiyo haitoshi, Uwoya alijimwambafai kuwa anaolewa na jamaa kutoka jijini Arusha, lakini mwisho wa siku aliishia kuzindua kipindi chake cha runingani ambacho hadi leo hakijaonekana.

 

ROSA REE

Msaii huyu alijikuta kwenye matatizo baada ya kusambaa kwa video ya wimbo alioshirikishwa na msanii wa Kenya ikimuonesha akishikwa sehemu nyeti za mwili wake.

Ilibidi kuitwa na Basata ambapo alipewa onyo kali, faini ya shilingi milioni mbili na kuomba radhi. Baadaye video hiyo iliondolewa kwenye Mtandao wa YouTube.

Makala: Neema Adrian

Leave A Reply