The House of Favourite Newspapers

Spoti Hausi LIVE: Binslum Afunguka Udhamini Wake Kwenye Soka la Tanzania

0

Mfanyabiashara Nasor Binslum ambaye anaidhamini Klabu ya Mbeya City amefunguka kuhusu udhamini wake kwenye klabu mbalimbali za soka hapa Tanzania huku akieleza kuwa yeye amekuwa mdau mkubwa wa soka tangu akiwa mtoto nyumbani kwao Tanga hivyo kuwa na mapenzi ya dhati ya kudhamini klabu za soka.

Akipiga stori na Spoti Hausi ya Global TV Online, leo Alhamisi kuanzia Saa 10:00 Jioni, nyumbani kwake dar es Salaam, Binslum ameeleza kuwa mbali na kuidhamini Mbeya City amewahi kuzidhamini Coastal Union ambayo ni timu yake tangu akiwa mtoto, Stand United na nyingine.

“Sikudhamini Coastal kwa sababu ya biashara, mimi ni shabiki wake na nilikuwa kiongozi kweny klabu hiyo hivyo lengo langu ilikuwa ni kuinua soka kwenye mkoa wangu na klabu yangu niipendayo,” alisema Binslum.

Aidha ameeleza kuwa hajawahi kuwa shabiki wa klabu kongwe za Simba wala Yanga huku akieleza kufurahishwa kwake na Mbeya City kwani wamekuwa na nidhamu kwa mdhamini huku akiahidi kufanya nao mambo makubwa zaidi katika kukuza soka.

Binslum ameitaka wizara ya michezo kusimamia uanzishwaji wa klabu zinazowakilisha mikoa ili kuzipa nguvu na kuachana na ushabiki wa Simba na Yanga jambo ambalo amesema linadidimiza soka la Tanzania kwani kila kiongozi amekuwa na maslahi kwenye klabu hizo huku akitolea mfano suala la kadi tatu za njano za Kagera Sugar zilivyoenda kwa Simba zikarudi KIagera.

Leave A Reply