The House of Favourite Newspapers

Staa Azimia Mazishi ya Mama Yake

0

Muigizaji mwenye asili ya Nigeria, Nkechi Blessings amemzika mama yake mzazi Mrs Gloria Obasi Oktoba 16, 2021, huku akiwa bado haamini kuwa mama yake amefariki!

Nkechi ambaye ameonekana kuathirika zaidi na kifo cha mama yake, siku ya mazishi alionekana kulia mbele ya mwili wa mama yake huku  akimuita na kumuomba  aamke.

Vdeo za mazishi ya mama yake zilionekana kusambaa mitandaoni huku zikithibitisha ni kwa namna gani Nkechi alijawa na huzuni. Katika kipande kimoja cha video kinamuonesha staa huyo akianguka chini na kuzimia wakati wa kuuaga mwili wa mama yake.

Na Bakari Mahundu, Dar

Leave A Reply