The House of Favourite Newspapers

Harmomize Afanya Bonge la Shoo Taifa, Stars Ikiichapa Burundi – Video

MSANII wa Bongo Fleva, Harmonize,  jana Jumapili, Septemba 8, 2019, aliungana na maelfu ya mashabiki katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kusherehekea ushindi wa timu ya taifa (Taifa Stars) kwa akiangusha bonge shoo uwanjani hapo baada ya Taifa Stars kuibuka mshindi kwa mikwaju ya penalti akiwa na mke wake Sarah.

 

Katika mechi hiyo, Tanzania iliibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 3-0 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dakika 120, ambapo huko Burundi  timu hizo zilitoka kwa mabao ya 1-1.

 

Baada ya ushindi huo na ulioifanya Stars isonge mbele katika michuano hiyo ya kuwania kusaka tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, Harmonize alipandisha mzuka na kuzama uwanjani kisha kuangusha bonge la shoo huku mashabiki wote wakimshangilia kwa nguvu.

TAZAMA TUKIO HILO

Comments are closed.