The House of Favourite Newspapers

StarTimes Yaichangia Serengeti Boys Sh Milioni 20

0

Mwandishi Wetu | Championi Jumatano | Dar es Salaam

STAR Media Tanzania kupitia kampuni yake ya StarTimes Tanzania imekabidi hundi ya Sh Milioni 20 kwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk. Harisson Mwakyembe ili kuichangia timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys inayojiandaa kushiriki Kombe la Mataifa ya Vijana.

StarTimes Tanzania ilitoa hundi hiyo katika harambee ya kuichangia Serengeti Boys iliyofanyika wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa JK Nyerere Convetion Center. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa StarTimes Tanzania, Wang Xiaobo alisema: “Tunafuraha kubwa sana kuichangia Serengeti Boys pamoja na serikali katika jitihada za kukuza michezo nchini,Tunaitakia timu kila la kheri iweze kuwakilisha vema nchi.”

Alisema mafanikio ya baadae yanategemea msingi mzuri na uwekezaji mzuri kwa vijana kwani ni hazina nzuri na tegemeo la kesho kwa kuliletea mafanikio taifa.

“Mbali na uchangiaji huu, tutaendelea kuchangia michezo mingine pamoja na shughuli za kiuchumi na kijamii ili kuisaidia nchi katika jitihada zake za kuleta maendeleo kwa wananchi,” alisema Xiaobo.

Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo, Mwakyembe aliishukuru StarTimes Tanzania na ameahidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika kufanikisha malengo yao na michezo kwa ujumla

Leave A Reply