The House of Favourite Newspapers

Sun Kika! Aliyepoteza Ndugu 7 Kimaajabu, Amtaja Angel Benard

0

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Sun Kika ameamua kuvunja ukimya na kuanika mazito kuhusu misukosuko ambayo familia yake imepitia hadi kiasi cha kutaka kukata tamaa.

 

Sun Kika ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya uitwao “My Hiding Place” (Maficho Yangu) ambao amemshirikisha mwimbaji mahiri wa Gospel nchini, Angel Bernard, amesema wimbo huo ni stori ya kweli inayohusu maisha yake, asingekuwa Mungu, pengine dada huyu asingekuwa hai hii leo.

 

Kwa nini My Hiding Place?

Akizungumza na Ijumaa Wikienda moja kwa moja kutoka nchini Marekani ambako yupo kwa sasa, Sun Kika amesema; Sun Kika anasema; “MY HIDING PLACE ni ushuhuda wa kweli wa maisha yangu. Nilizaliwa nikiwa liwazo kwa wazazi wangu.

 

“Kabla ya kuzaliwa kwangu wazazi wangu waliopoteza watoto saba. Nimepoteza kaka na dada waliokufa kati ya mwaka mmoja hadi miaka nane, ambao walikuwa wakipoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha bila kufahamu ugongjwa uliyokuwa ukiwamalaiza, naweza kusema walikufa kimaajabu.

 

“Baada ya mimi kuzaliwa, wazazi wangu hawakuwa na tumaini kabisa iwapo ningeweza kuishi, pengine na mimi ningeondoka duniani lakini nimemwona Mungu akipigana vita vyangu, akiniokoa na kifo mara nyingi, AMEKUWA MAFICHO YANGU. Tunamtumikia Mungu mwenye uwezo, anaweza kufanya mengi tunayoweza kumwomba na kufikiria” amesema Sun Kika ambaye ni mtoto wa Mchungaji Cephia Maranatha.

 

Mwimbaji huyo ameweza kutengeneza combination nzuri na mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Angel Benard anayetamba na nyimbo zake ikiwemo SITEKETEI.

Kwa nini Angel Bernard?

Nimemshirikisha Angel Bernard kwa sababu kwanza ni mwimbaji mzuri, ninapenda uimbaji wake. Wakati naanza kazi hii ya uinjilishaji kwa njia ya nyimbo nilitamani sana siku moja niwe kama yeye au nifanye naye kazi, kwa hiyo ninaamini ndoto yangu imetimia kupitia My Hiding Place.

 

Kwa nini Marekani?

Video ya wimbo huu imefanyika nchini Marekani, kwanza ni kwa sababu sote tupo marekani kwa sasa hivyo ilikuwa rahisi kukaa na kufanya kitu cha pamoja tukiwa pamoja. Janga la corona pia limechangia lakini hata locations kwa hapa Marekani inakuwa rahisi zaidi na zinavutia, hata productions zinakuwa za kiwango cha juu, lakini hata nyumbani Afrika kazi nyingi nzuri zinafanyika na kwa kiwango cha juu.

 

Mipango Mingine?

Baada ya MY HIDING PLACE, kwa sasa najiandaa kuachia albamu yangu, hivyo nafanya recording na mambo mengine ya production ili kuikamilisha, ikishakuwa tayari itaianika ili tuendelee kumsifu Mungu kwa njia ya nyimbo na kuitangaza injili. Baada tu ya corona kuisha tutatua Tanzania na Angel kufanya tour ya kuutangaza wimbo huu, lakini kwa sasa niwasihi mashabiki wangu waitazame video ya wimbo wangu huu kupitia YouTube channel yangu ya Sun Kika.

 

Leave A Reply